HUSSEIN MWINYI; ZANZIBAR MUACHE TABIA YA MUHALI
Akizungumza na wananchi pamoja na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi wa Mkoa wa Mjini Kichama hapo Makao Makuu ya Chama hicho Mkoa Amani, katika ziara ya kuwashukuru, alisema bado hajaridhishwa na utendaji wa jeshi la Polisi katika kushughulikia kesi za udhalilishaji wa kijinsia.
Rais Dk. Mwinyi ambaye pia, ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) alisema yapo malalamiko kutoka kwa jamii kwamba jeshi la Polisi limekuwa likifanya upatanishi wa kusuluhisha wa kesi hizo katika vituo vya Polisi na kumalizana kienyeji.
Alifahamisha hizo sio kazi za jeshi la Polisi kwa mujibu wa sheria ambapo wanatakiwa kuhakikisha wanatayarisha kesi kwa kufanya upelelezi na kuzipeleka mbele kwa hatua nyengine.
Hivyo, Rais Dk. Mwinyi alitumia fursa hiyo kuwapongeza Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kwa kufanya marekebisho mazuri katika sheria za udhalilishaji ambapo mtuhumiwa wa makosa hayo atakuwa akinyimwa dhamana.
Post a Comment