CARLINHOS AONDOKA YANGA, AVUNJA MKATABA
NA ALI KAMWE;
Rekodi za Carlinhos kwenye VPL msimu huu
Asisti: 3
Mabao: 3
Mechi: 9
Taarifa zinasema hii ilikuwa mara ya tatu kwa Carlinhos kushinikiza kuvunja mkataba wake na Yanga
Awali alidai anapata changamoto ya chakula hivyo Uongozi wa Yanga umsafirishe mkewe aje Tanzania la sivyo angevunja mkataba. Yanga wakafanya hivyo.
Mke akaja Dar. Maisha yakaendelea.
Baadae Carlinhos akaanza kusumbua kinidhamu. Kupenda kujitenga na kutaka huduma 'spesho' tofauti na wachezaji wenzake wanapokuwa kambini
Awamu hii, Uongozi ukamuita Wakala wake kuja kusuluhisha hili.
Jaribio la mwisho ni pale mkewe aliposafiri kurudi Angola kwa ajili ya kwenda kujifungua.
Kilio cha 'chakula na kuwa mbali na Familia' kikarudi kwa Carlinhos. Safari hii akagoma kucheza kwa madai ni majeruhi.
Taarifa zinasema kila daktari wa timu alipompangia ratiba, hakuripoti kwa wakati. KITU KIMOJA ALICHOKUWA ANAKITAKA NI KUVUNJA MKATABA WAKE.
Uongozi ukaridhia kuvunja mkataba kwa makubaliano. Kama Atapata Timu Tanzania, Carlinhos atatakiwa kuilipa Yanga kiasi cha dola 200,000 (Zaidi ya Tsh Mil 450).
Inadaiwa pia makubaliano mengine ya kuvunja mkataba ni kuwa kama Carlinhos atapata timu nje ya Tanzania, atatakiwa kuilipa klabu robo tatu ya 'signing fees' aliyochukua.

MAONI YANGU • Kwa kuthamini kipaji cha Carlinhos, Uongozi wa Yanga ulifanya kila kitu kwa ajili ya kuhakikisha anacheza soka katika mazingira mazuri hapa Tanzania
Lakini moyo wa Carlinhos ulishaingia kiza. Hakutana kuendelea kubaki Yanga. Alifanya kila kitu kuondoka.
Ni nafasi sasa kwa uongozi wa Yanga Kujifunza jambo katika USAJILI WAO unaokuja.
Wanatakiwa kufanya tafiti ya kutosha ya kiufundi, kinidhamu, kimazingira na tamaduni kwa wachezaji wanaowatoa kutoka nje ya Tanzania.
Carlinhos sio wa kwanza wala hatakuwa wa mwisho.
Wako wachezaji/makocha wengi duniani wamewahi kuathirika na mazingira/tamaduni za mataifa wanayokwenda kucheza/kufundisha nje ya kwao.
Wanachotakiwa kufanya viongozi wa Yanga kujiridhisha katika maeneo mengi mbali na kuomba tu 'Clip za YouTube' kutoka kwa Mawakala wa wachezaji.

Post a Comment