SERIKALI YAJIZATITI KUIMARISHA UFUNDISHAJI SOMO LA MICHEZO
Serikali imejizatiti kuimarisha ufundishaji wa somo la michezo shuleni na na kuongeza ubora wa mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma kwa Shule za Msingi Tanzania (UMITASHUMTA) na Umoja wa Michezo wa Shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA).
Hayo yameelezwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa James Mdoe Jijini Dodoma ambapo amesema Serikali inaandaa mashindano hayo ikiwa ni mwendelezo wa ufundishaji wa somo hilo katika shule.
"Serikali imeamua kutilia mkazo ufundishaji wa michezo shuleni kwa kutambua kuwa michezo ni sehemu muhimu katika makuzi ya afya na akili kwa vijana wetu " amesisitiza Profesa Mdoe.
Naibu Katibu Mkuu huyo ameyataja manufaa ya mashindano hayo makubwa kuwa ni pamoja na kuwajengea vijana uwezo wa kujiamini katika masuala mbalimbali ya kitaaluma na maisha, kuwajenga katika stadi za ubunifu, kuwajengea mazingira ya upendo, kufahamiana na kujenga misingi bora ya mshikamano na umoja wa Kitaifa.
Ameongeza pia kuwa michezo inawasaidia vijana kumudu mbinu za ushindani katika masuala mengi wanayokutana nayo katika maisha ya kila siku.
Naye Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Profesa Riziki Shemdoe amesema mashindano hayo yatafanyika Mkoani Mtwara katika uwanja wa Nangwanda Sijaona na yatazunduliwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa Juni 8, 2021.
Profesa Shemdoe amesema mwaka huu mashindano ya UMISETA yanashirikisha wanafunzi 3800 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar na wanafunzi 3600 kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara wanashiriki UMITASHUMTA.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi amesema Serikali itaendelea kuboresha mashindano hayo ili yawe kituo cha kukuza vipaji kwa kuwaandaa na kuwauza kimichezo.

Post a Comment