HOTUBA YA RAIS SAMIA JANA MEI 5,2021
“Nashukuru kwa kukaribishwa kuhutubia Bunge tena kikao cha pamoja cha Mabunge mawili, najua sio kila Rais anayekuja hapa anapewa hii fursa nimefarijika sana, Tanzania tuna Bunge moja, kwangu ndio mara ya kwanza kuhutubia Bunge lenye chemba mbili, ni heshima iliyoje.
Uamuzi wenu wa kunipa fursa hii ni kielelezo cha thamani mnayoupa umoja wetu, namshukuru Rais Kenyatta ni miongoni mwa Viongozi wa kwanza kabisa aliyenipigia simu kunipa pole kwa msiba wa Hayati Magufuli na akaja pia Dodoma kutufariji." Rais SSH

Sisi ni Majirani hata wanyamapori wetu ni Ndugu na ni Majirani, kuna wanyama wanakuja kupata mimba Kenya wanazalia Tanzania, ingekuwa wanyama wana Uraia wangekuwa Raia wa wapi? hata Tausi wetu waliopo Ikulu Tanzania wana Ndugu zao Ikulu Nairobi” Rais SSH
“Tumekuwa na mazungumzo mazuri na yenye kuamsha matarajio makubwa sana kwa Nchi zetu mbili, kwa yale tuliyotofautiana hayakuwa na misingi ila tu ni mitazamo tofauti ya Watu, uchungu wowote uliojitokeza ulikuwa uchungu wa uzazi na sio wa maradhi.
Uchungu wa uzazi unaishia kuleta Mtoto na unaleta furaha kwenye Familia lakini uchungu wa maradhi unaishia kwenye kifo, sisi (Tanzania na Kenya) tunapokerana huo ni uchungu wa uzazi, tukae tuzungumze tupate Mtoto Amani tuendelee na uhusiano wetu." Rais SSH

“Chini ya uongozi wangu, tutafanya kila tunachoweza ili kuimarisha uhusiano wetu, Dira ya Serikali yangu ni kudumisha ya awamu iliyopita na kuendeleza mapya, kama kuna ambalo linalega au uhusiano wetu unasuasua nimekuja kuyanyoosha yale yaliyojipindapinda.
Kenya ndio Nchi ya kwanza kwa mimi kufanya ziara rasmi, nilienda Uganda kusaini mkataba ila haikuwa ziara rasmi, ziara yangu ya kwanza rasmi tangu kushika Uongozi nimeanzia Kenya na sio kwasababu ni karibu kijiografia ila ni kwasababu ya umuhimu wa Kenya kwa Tanzania” Rais SSH

“Binafsi huwa nashangazwa sana na wale ambao wanadhani kuwa eti Kenya na Tanzania ni washindani na kwamba uhusiano wetu unapaswa kuwa wa kukamiana na mbaya zaidi ni kule kuamini kwao kwamba hilo linawezekana tu mmoja wetu kumwangusha mwenzake.
Watu wanaoamini Tanzania na Kenya ni Washindani ni wenye choyo, maono mafupi na akili mbovu, bahati mbaya Watu hawa wapo kwenye pande zote Kenya na Tanzania na wapo ambao wapo kwenye Serikali zetu na Wanasiasa, bahati nzuri sio wengi ndio maana uhusiano wetu unadumu.
Kwa yeyote anayefikiria kuleta uhasama baina yetu, ujumbe wangu kwao ni kwamba Tanzania na Kenya, tulikuwepo, tupo na tutaendelea kuwepo, iwe kiangazi iwe masika Tanzania na Kenya tutaendelea kuwepo." Rais SSH

Post a Comment