EPSODE 5 NA KANKWI WA KANKWI
Basi baada ya kupewa barua tukapanga safari ya kwenda bumbuli,tulikuwa mimi,mume wa idda(mshirika jina utani) na dada idda na mjomba angu mmoja hivi ni mtoto wa dada angu mwingine tukasafiri safari tuliiona ndefu kwasababu ilikuwa ni siku ya kwanza na ugeni wa mazingira.
Mungu akatusaidia tukafika salama mpaka ofisi ya mkurugenzi bahati mbaya hatukumkuta ikabidi tulale ili asubuhi tuonane nae.
Tukalala kesho yake asubuhi tukafika na tukamkuta pale Alinipokea vizuri mkurugenzi na wasaidizi wake na kunipa ushirikiano wote basi nikajaza jaza mafomu pale yote nikamaliza nikaambiwa kituo chako cha kazi ni hospital hivo utakuwa chini ya ofisi ya DMO,akaitwa DMO pale akapewa taarifa zangu akanipokea pia tukamaliza pale na nikaomba siku 14 za kujipanga nyumbani ili nije kuanza kazi rasmi.
Safari ya kurudi Dar ikaanza na tukafika Dar salama. Zile siku 14 zikaisha nikaja kazini rasmi nilipokewa vizuri nikatafutiwa mahali pa kukaa na daktari mfawidhi katika hosp ya bumbuli mzee wangu Erasto Mungu ambariki pia,nikatambulishwa kwenye timu ya CHMT wakanipokea vizuri maisha yakaendeleaa na kufanya kazi za watu.
Changamoto zilikuwepo mazingira ya huku ila nilipata msaada pale ninapokwama hali ya hewa baridii mnoooo.
Basi ukapita mwaka 2018 nikaona mbona naeza kuishi tu kwahio wazo lile la kuhama likapotea mwaka 2019 nao ukaisha naona maisha fresh tu nikaanza kuwaza kuoa sasa nikasema nitafute msambaa wangu mie tuishi lkn kila nikichek sioni nikavuta subiraa basi mwaka 2020 ndio huku na huku ndio nakutana na Jesca.
Nakumbuka niliweka nadhiri kwa Mungu kuwa anisaidie nikifika umri fulani ambao ni 35 niwe nimeshakutana na mke wangu na niweze kumuoa na sio sogea tuishi.
Basi ikawa hivo Jesca kwa kifupi tunafahamiana tangu watoto huko kijijini lkn hatukuwahi kufikiri leo hii tungeoana ila baada ta muda mrefuu kupita miaka mingi tangu 1998 tukaja kukutana 2020 huko facebook siku tu nilipost picha akakoment Dm na hapo ndipo tulianza kuwasiliana na tukaanzisha mahusiano mpaka kuja kuoana 2021 tarehe 10 April.
Mungu ni mwema tunafuraha familia zetu zinafuraha na hata ndugu zetu na hata marafiki nyinyi pia mnafuraha na mnatupongeza sana TUNAWASHUKURU sana.
Post a Comment