ANAANDIKA AMAN MARTINS PART 1
Februari 2010, Haji alifikishwa mbele ya Hakimu Benadicta Beda na kusomewa mashtaka 6 yaliyohusu utapeli wa magari.
Siku hiyo Haji alikosa dhamana, akarudishwa rumande, nduguze na wengine waliojua ukweli walilia, maadui zake walishangilia na kudhani "AMEKWIIISHAA".
Ninayo picha ya siku ile naitazama kisha namtazama Haji wa leo nasema kweli mpewa hapokonyeki.
Namuomba radhi ndugu @hajismanara kwa kukumbusha stori hii ambayo yaweza kuwa tukio lililomuumiza zaidi maishani, lakini hapana shaka ataelewa lengo langu.
Kesi ya utapeli wa magari ilikuja Haji akiwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM mkoa wa DSM, na kutokana na tuhuma zile alijiuzulu. Baadae, kesi iliisha, Haji akasamehe na kusafishika, kwani kama angekuwa na hatia leo angekuwa Segerea na sio Simba.
Ukubwa wa kesi ile, ulitosha kabisa kumuondoa mtu kwenye ramani, lakini haikuwa hivyo, ule ulikuwa moto wa kuing'arisha dhahabu ya leo, yenye thamani kubwa mitaa ya Msimbazi.
Nakurudisha nyuma : Haji alizaliwa kwenye familia ya 'super star' Sunday Manara, akapelekwa shule, Afrika Kusini ndiko alisoma masuala ya Mawasiliano, akarudi Tanzania.
Nakurudisha nyuma : Haji alizaliwa kwenye familia ya 'super star' Sunday Manara, akapelekwa shule, Afrika Kusini ndiko alisoma masuala ya Mawasiliano, akarudi Tanzania.
Alifanya kazi redio Uhuru kama mtangazaji na muandishi wa habari za michezo na siasa, kabla ya kwenda CCM na kukutana na kisa nilichotaja pale juu.
Baadae aliibukia @simbasctanzania.
NI #CHAMP : Miaka aliyozaliwa dhana potufu kuhusu watu wenye ulemavu wa ngozi zilikuwa nzito kweli kweli, kaa naye akusimulie yote aliyopitia. Nisiende huko nikaingia ndani sana, tubaki hapa kwenye mpira.
NI #CHAMP : Miaka aliyozaliwa dhana potufu kuhusu watu wenye ulemavu wa ngozi zilikuwa nzito kweli kweli, kaa naye akusimulie yote aliyopitia. Nisiende huko nikaingia ndani sana, tubaki hapa kwenye mpira.
Kwa namna alivyoipa thamani kazi yake kama msemaji, hamasa aliyotoa na kuikuza brand ya @simbasctanzania licha mishale mingi mingine akipigwa ndani ya Club yake : niambie Haji sio #Champ nikuite mchawi.
Tunaweza kutofautiana kwenye ushabiki na kile tunachoamini, lakini tusikimbie kivuli cha ukweli na weledi kwenye kile anachokifanya.
Mie shabiki wa @yangasc, lakini naiona hamasa kwenye uvungu wa maneno ya Haji yanayonikera, kwenye sura yake naliona tumaini na somo kubwa kwa watu ambao wangeweza kuambiwa "Huwezi" kutokana na jinsi walivyoumbwa au njia walizopita.
"MANARA; NEXT POST NTAELEZEA REPOST HII NA MTAZAMO WANGU
Post a Comment