AMKA NA BWANA LEO 31
KESHA LA ASUBUHI
JUMATATU, MEI, 31, 2021
SOMO: MALAIKA WETU WALINZI
Kwa kuwa Wewe BWANA ndiwe kimbilio langu; umemfanya Aliye juu kuwa makao yako. Mabaya hayatakupata wewe, Wala tauni haitaikaribia hema yako. Kwa kuwa atakuagizia malaika zake, Wakulinde katika njia zako zote.
Zaburi 91:9—11.
Malaika wamepangwa kuitazama kila familia. Kila mtu anapewa ulinzi wa malaika mtakatifu. Malaika hawa hawaonekani, lakini wakati mwingine wanaonesha nuru yao kwa udhahiri kabisa hadi inatambuliwa. Ninaamini huu ndio ufunuo uliooneshwa. Udhihirisho huu unakufundisha kwamba Bwana anakupenda, na kwamba malaika Zake wanakulinda. Unalindwa kwa uwezo wa Mungu.
Mambo mengi yafananayo na hayo yatachukua mkondo wake. Udhihirisho huu wa nuru ni kwa ajili ya kukutia moyo, kama unavyosema umefanya hivyo, ili ufanye mambo sahihi. Umeona sehemu ndogo ya nuru ya Mungu, na hebu jambo hili lihamasishe moyo wako, ukikufanya uwe mwenye shukrani. Sisi sote tunapaswa kuwa wenye shukrani wakati wote kwa ajili ya ukweli kwamba malaika wa mbinguni wanatulinda kila wakati. Watu wengi sana kama wangeona nuru ambayo umeona wangefurahi na kuwa wenye shukrani.
Unapoyachunguza maandiko, ukijaribu kuwa sahihi na kufanya mema, malaika wanaozilinda hatua zako wanafurahia. Malaika wa mbinguni wanakuja kwa namna ambayo inaonekana kwa wale ambao wanaukubali ushahidi wa ukweli kujaribu kuutii. Na ikiwa malaika hawa hawaonekani daima, unapaswa kukumbuka kwamba wapo kama kawaida, isipokuwa tu macho yako ya kibinadamu hayana nguvu ya kuiona nuru yao...
Shida kubwa kwetu sote ni kwamba hatuchukui muda wa kufikiri kwamba viumbe wa mbinguni wapo karibu nasi, ili kutusaidia katika kila shauku yetu ya kufanya mambo sahihi. Nuru ya mbinguni imekuja karibu sana nawe. Umepewa ushahidi kwamba Bwana anakupenda na anakujali. Unaweza kuwa na ujasiri, na kuhisi kwamba unapokea nguvu na neema ya kufanya mema yote ambayo unaweza kuyafanya....
Mshukuru Bwana, moyo wako umeshawishiwa, kwasababu umependelewa kuona kaisi cha miale ya nuru kutoka kwa wajumbe wa mbinguni. Unaweza kuona ni kwa kiasi gani unaweza kufanya ili kumsaidia mama yako na wanafamilia wengine katika familia yako. Mkristo ni yule ambaye anajifunza kila siku, akitekeleza majukumu madogo ya maisha, akibeba mizigo ya wengine. Kwa namna hiyo utakuwa na umoja pamoja na Kristo.
—Barua ya 82, Mei 31, 1900,, kwa Elsie Atkins, mshiriki wa kanisa kijana nchini Australia.
Post a Comment