MUONGOZO WA KUSOMA BIBLIA LEO 31

LESONI, MEI 31

SOMO: TAIFA KUU, HODARI.... 



Siyo tu kuwa Mungu alimwahidi Ibrahimu kuwa kupitia kwake jamaa zote za dunia zitabarikiwa; bali Mungu alitamka pia kwamba atamfanya kuwa “taifa kuu, hodari” (#Mwanzo 18:18;# soma pia #Mwanzo 12:2,# #Mwanzo 46:3.#) —ahadi itolewayo kwa mzee aliyeoa maana ambaye umri wake wa kuzaa ulishapita. Naam, wakati Ibrahimu hakuwa na uzao, wala hakuwa na mwana, Mungu alimpatia ahadi hizo. 



Hata hivyo, ahadi hii haikutimilika kwa ukamilifu wake wakati Ibrahimu akiwa bado hai. Wala Isaka au Yakobo hawakuona utimilifu wake. Mungu alirudia ahadi hiyo kwa Yakobo, kukiwa na maelezo ya ziada kuwa ahadi hiyo ya kuwa “taifa kuu, hodari” itatimilika huko Misri (#Mwanzo 46:3#), japo Yakobo hakuishi kushuhudia utimilifu wake. Ndipo hatimaye ahadi hiyo ikatimilika. 



Kwa nini Mungu alikusudia kuunda taifa maalumu kutoka katika uzao wa Ibrahimu? Je Mungu alitaka kuwa na nchi nyingine yenye watu wa taifa maalumu? Taifa hili lilikusudiwa kutimiza kusudi gani? Soma #Kutoka 19:5, 6;# #Isaya 60:1—3;# na #Kumbukumbu 4:6—8# na katika mistari wazi hapa chini andika jibu lako:



Maandiko yanaonesha bayana kuwa Mungu alikusudia kuyavuta mataifa mengine kwake kupitia ushuhuda wa Israeli, taifa ambalo kwa kupitia baraka zake lilikuwa linakwenda kuwa taifa lenye furaha, afya na takatifu. Taifa hilo lilikuwa linakwenda kudhihirisha baraka inayopelekana na utii kwa mapenzi ya Mungu. Matokeo yake watu wengi wa dunia watavutwa kumwabudu Mungu wa kweli (#Isa. 56:7#). Hivyo, usikivu wa wanadamu utavutwa kwa Israeli, Mungu wao, na kwa Masihi, ambaye angetokea kati yao, Mwokozi wa ulimwengu. 



“Wana wa Israeli walipaswa kutawala eneo lote Mungu alilowapatia. Mataifa yaliyokataa ibada na huduma kwa Mungu wa kweli yalipaswa kufukuziwa mbali na kuangamizwa. Lakini ilikuwa ni mpango wa Mungu kuwa ufunuo wa tabia yake watu wa Israeli wavutwe Kwake. Injili ya mwaliko ilikuwa itolewe kwa dunia yote. Kupitia mafundisho ya huduma za kafara Kristo alipaswa kuinuliwa juu mbele za mataifa, na wote watakaomtazama wapate kuishi.” —Ellen G. White, Christ’s Object Lessons, uk. 290.



Je unaweza kuona ulinganifu gani kati ya kile BWANA alichotaka kufanya kupitia Israeli na kile anachotaka kutenda leo kupitia kwa kanisa letu? Iwapo upo, ni ulinganifu gani? Soma #1 Petro 2:9#.


Je una taarifa unaitaji kuwekwa kwa kurasa zetu tutafute kwa 0621663340

No comments