NA MALISA GJ PART 2

Ikumbukwe Mkoa wa Geita ulianzishwa kusudi Chato iwe Makao Makuu. Ikakosa vigezo. Geita mjini ikaonekana ndiyo yenye sifa za kuwa Makao Makuu ya Mkoa mpya wa Geita. Hii ilikuwa 2010. Sasa 11 years later Chato ati ina vigezo kuwa Makao Makuu ya Mkoa wake wenyewe? Are we serious with our development? Really?

Na Rais wetu mpendwa SSH tunataka kweli kumtwisha zigo la kuamua jambo hili na controversy zake? Elimu haina mwisho. Mimi kama kuna vigezo naomba viorodheshwe. Labda ndiye sina taarifa. Ila so far Hoja ya kuwaletea maendeleo Kakonko, Biharamulo, Ngara na Muleba inayokatwa vipande ninazikataa. Mkoa unaweza kuleta maendeleo gani kwa Wilaya yake wakati Mkoa unategemea bajeti ya Serikali Kuu.

Mkoa una mapato gani zaidi ya kutumia kodi? Lets be serious. Maendeleo yanatokana na uwekezaji na uwezeshaji kwa wananchi. Siyo watumishi wa Serikali tena baadhi bila maadili wanaweza kuishia kuwabugudhi wananchi badala ya kuwa msaada.

Njia pekee kumuenzi Hayati Magufuli ni kurekebisha mambo ambayo kama binadamu hakufanya vizuri. Mengine yote ni ubinafsi. Na kufifisha sifa zake katika historia ya nchi hii. Tumuache apumzike.

Miundombinu iliyowekwa Chato siyo kigezo kuunda mkoa hapo. Tuikamilishe na kuitafutia matumizi mbadala ya kitaifa. Mfano Airport ya Chato inaweza kufanywa Hub ya kilimo cha contract floriculture na horticulture (kilimo mkataba cha maua na mbogamboga) ili tuwe na ndege za mizigo kuja kubeba mbogamboga, maua na maziwa.

Hospitali ya Kanda Chato sio kigezo cha kuipa Chato hadhi ya mkoa. Naomba tutathmini kwanza maendeleo ya hospitali ya Mloganzila. State of the Art buildings only 40km away from Dar City Centre na Muhimbili. Mojawapo ya mafanikio makubwa ya Awamu ya nne.

Lakini Angalia changamoto zake. Uhaba wa madaktari hadi leo. Sasa hao specialist doctors watakaokubali kuishi Chato mtawalipa fedha kiasi gani? A hospital is not just buildings. Its manpower resources and the economy surrounding it.

Katika dhana ya mipango miji na maendeleo ya makazi lazima vigezo vyote hivyo kuangaliwa. Kwa uelewa wangu Chato haina vigezo. Tusidanganyane.


No comments