UOVU MWINGINE UTOKANA NA WEWE NA SIO SHETANI
MKRISTO AUMBUKA KWA KUWA HAJUI MAOVU HUTOKEA WAPI HASA...?
😁😁😁😁
Siki kila ovu hutokana na Shetani!
Maovu mengine hutokana na uchafu wa nafsi yako mwenyewe kisha unamzingishia Shetani kwa kuwa ndiye jalala la kutupiwa LAWAMA ZOTE MBAYA..!!!
Mathayo 15:11,15-20
[11]Sikilizeni, mfahamu; Sicho kiingiacho kinywani kimtiacho mtu unajisi; bali kitokacho kinywani ndicho kimtiacho mtu unajisi.
[15]Basi Petro akajibu, akamwambia, Tueleze mfano huo.
[16]Yesu akasema, Hata sasa ninyi nanyi mngali hamna akili?
[17]Hamjafahamu bado ya kuwa kila kiingiacho kinywani hupita tumboni, kikatupwa chooni?
[18]Bali vitokavyo kinywani vyatoka moyoni; navyo ndivyo vimtiavyo mtu unajisi.
[19]Kwa maana moyoni hutoka mawazo mabaya, uuaji, uzinzi, uasherati; wivi, ushuhuda wa uongo, na matukano;
[20]hayo ndiyo yamtiayo mtu unajisi; lakini kula kabla hajanawa mikono hakumtii mtu unajisi.
JE, ULIMSIKIA SHETANI AKITANJWA HAPO?
PAULO NAYE ATAJA MATENDO YA MWILI HAJAYAITA KUWA NI MATENDO YA SHETANI! 👌👌👌
Wagalatia 5:16-21
[16]Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili.
[17]Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka.
[18]Lakini mkiongozwa na Roho, hampo chini ya sheria.
[19]Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi,
[20]ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi,
[21]husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu.
NAFSI YAKO IKUTUME KUZINI AO KUNYWA POMBE KISHA MZIGO HUU UMBEBESHE SHETANI????
😁😁😁😁
HATA SHETANI NAYE ATAKATAA KUUBEBA MZIGO WAKO!
Wagalatia 6:5
[5]Maana kila mtu atalichukua furushi lake mwenyewe.
UTAMANI VYA WATU UMZINGISHIE SHETANI?
Yakobo 1:13-15
[13]Mtu ajaribiwapo, asiseme, Ninajaribiwa na Mungu; maana Mungu hawezi kujaribiwa na maovu, wala yeye mwenyewe hamjaribu mtu.
[14]Lakini kila mmoja hujaribiwa na tamaa yake mwenyewe huku akivutwa na kudanganywa.
[15]Halafu ile tamaa ikiisha kuchukua mimba huzaa dhambi, na ile dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti.
😁😁😁😁
۞ وَمَا أُبَرِّئُ نَفْسِي ۚ إِنَّ النَّفْسَ لَأَمَّارَةٌ بِالسُّوءِ إِلَّا مَا رَحِمَ رَبِّي ۚ إِنَّ رَبِّي غَفُورٌ رَّحِيمٌ
(YUSUF - 53)
NAMI sijitoi lawamani. Kwa hakika nafsi ni mno kuamrisha maovu, isipo kuwa ile ambayo Mola wangu Mlezi aliyo irehemu. Hakika Mola wangu.
Post a Comment