SIKU ZA MWISHO
JE, KUNA MTU YEYOTE ATAKAYETAMBUA SAA YA KUKATA MANENO IMEFIKA???
Kabla ya gharika , baada ya Nuhu kuingia ndani ya safina , MUNGU alimfungia ndani ya sAfInA na kuwafungia nje wale wasiomcha MUNGU , Lakini kwa siku saba , bila kujuwa kuwa mwisho wao ulikuwa tayari umeamuliwa, watu waliendelea na maisha yao ya kutojali, kupenda anasa na kudhihaki maonyo ya hukumu iliyokuwa imekaribia sana.
👉🏻Mwokozi anasema: Ndivyo itakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu.(YESU )
Mathayo 24:39.
Kimya kimya , bila kuonekana kama mwivi wa usiku wa manane , itakuja saa ya kukata maneno itakayoamua mwisho wa maisha ya kila mtu, kuondolewa kwa mara ya mwisho kwa toleo la rehema kwa Wanadamu wenye hatia.
🤔Wakati mtu wa biashara amezama katika kutafuta faida, wakati mpenda anasa anatafuta kujifurahisha nafsi yake, wakati Binti wa mitindo anapanga mapambo yake, huenda ni katika saa iyo hiyo , MHUKUMU wa dunia yte atakapotamka maneno haya: UMEPIMWA KATIKA MIZANI NAWE UMEONEKANA KUWA UMEPUNGUA.
👉🏻Dhiki Kuu inatunyemelea polepole,. Jua linaangaza huko mbinguni, likipita katika njia yake kama kawaida, na mbingu zingali zikitangaza utukufu wake MUNGU . Watu wangali bado wanakula na kunywa, wakipanda na kujenga, wakioa na kuolewa. Wafanya biashara bado wanaendelea kununua na kuuza. Watu wanapigana vikumbo, wakigombania nafasi za juu sana.
👉🏻wapenda anasa bado wanajaa kwenye majumba ya michezo⚽⚽🏸🏋🏻🏀🏌🏻🥊, mbio za Farasi🏇🏻🏇🏻🏇🏻🏇🏻 na kwenye kumbi za michezo ya kamari🌆.
Misisimko mikubwa imeenea kila mahali, lakini saa ya kufungwa mlango wa rehema inakaribia sana, na kila kesi karibu sana itakatwa milele.
Shetani anajuwa kwamba wakati wake ni mchache. Amewaweka mawakala wake wote kazini ili watu wapate kudanganywa, kughilibiwa akili zao, kutingwa na shughuli, na kuvutiwa sana mpaka siku ya majaribio itakapofika mwisho wake na mlango wa rehema kufungwa milele.
(ChS 51, FE 335) GC 491
Waangalie ndugu zangu waadventista WASABATO wa siku ya saba walivyolala, wanasubiri Neema kuokoa, jambo ambalo hawatolipata kutokana na uvivu wa kumtafuta MUNGU nafasi ingalipo.
Leo Wasabato wa siku ya saba hawajali hata ibada. Waangalie huko makanisani jinsi asubuhi wanavyojazana makanisani siku ya SABATO , jioni siku ya SABATO hawaonekani ibadani. Tembelea kwenye kumbi za starehe siku ya sabato, utawaona watoto wa MUNGU wakiwa wamechanganyikana na walimwengu wakishirikiana kuzomea na kupiga yowe na kusikitika bila sababu.,⚽⚽. Watu wa Mungu wamekuwa mateka wa shetani bila wao kujuwa.
👉🏻Tembela nyumba za washiriki masaa ya sabato jioni, wote wamekaa wakiisikiliza TV, michezo ya maigizo ya mapenzi, umbea, uongo, uzandiki, Taarabu, ulevi, uchoyo nk ndiyo wanayojilisha na watoto wao mida ya masaa ya SABATO, kweli tutaokolewa????🤔🤔🤔, hatuwezi kuokolewa ndugu zangu, kwahizi dhambi za makusudi usitegemee kuokolewa.
Mda wa kufungua sabato, watu wa Mungu hawaonekani ibadani, wako bize huko nje kuiharifu SABATO ya MUNGU , Hivi tupo tayari kwaajili ya kuihama hii dunia????🤔🤔🤔, bado hatujawa tayari.
Waangalie waadventista watunza sabato leo jinsi ambavyo tumekuwa washabiki wa viongozi wa kidini makanisani badala ya kuwa mashabiki wa KRISTO. Neno la MUNGU limedharauliwa kuliko kawaida, MUNGU amenyang'anywa utukufu na wajiitao WACHUNGAJI na Wazee wa makanisa. Hali ni mbaya mno kati ya waumini.
Wengi wa waumini wanaujuwa ukweli wa leo, lakini wamekuwa mateka wa viongozi na hawako tayari kuiinua bendera ya YESU juu na badala yake wameitupa chini kuinua bendera nyeusi kati ya waumini wenzao, Hawa nao wanajiandaa kuokolewa???🤔🤔
Watu hawataki Ukweli usemwe, hao ni viongozi wa makanisa waliopewa dhamana ya kulichunga kundi, na hata ukisema utaambiwa, KANISA HILI LINAONGOZWA NA YESU NA ATALIFIKISHA BANDARINI SALAMA, WEWE UMEZALIWA NA UMELIKUTA KANISA NA UTAKUFA UTALIACHA LIKIENDELEA😭😭, Hizi ndizo kauli za watu wa MUNGU , yaani hata dhambi inapaliliwa ili isisemwe na inaundiwa misemo ya kukatisha tamaa.
Kweli YESU anakuja. Kabla hajaonekana mawinguni tutashuhudia mengi ndani ya kanisa na nje ya kanisa.
Simama na MUNGU pekee
Muamini Kristo wake
Simama juu ya Neno lake tu
Muombe MUNGU akuongoze yeye peke yake.
Lakini mwisho wa mambo yte umekaribia, basi iweni na Akili.
Post a Comment