AMKA NA BWANA LEO 14
KESHA LA ASUBUHI
JUMATANO, APRILI, 14, 2021
SOMO: UWE MJUMBE WAKE
Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe. Aaminiye na kubatizwa ataokoka asiyeamini, atahukumiwa.
Marko 16:15, 16
Watenda kazi katika kazi ya Mungu wanaweza kujifunza somo la thamani katika maelekezo aliyoyataoa Yesu kwa wale wanafunzi sabini na kupitia uzoefu wao. Wanafunzi hawa walitumwa katika miji kazi ya Yesu, ilikwamba watu waandaliwe kupokea ukweli kuu ambazo angewapatia.
"Basi, baada ya hayo Bwana aliweka na wengine, sabini, akawatuma wawili wawili wamtangulie kwenda kila mji na kila mahali alipokusudia kwenda mwenyewe. Akawaambia, Mavuno ni mengi, lakini watenda kazi ni wachache; basi mwombeni Bwana wa mavuno apeleke watenda kazi katika mavuno yake. Enendeni, angalieni, nawatuma kama wana kondoo kati ya mbwa-mwitu.” (Luka 10:1—3)...
“Na mji wo wote mtakaouingia, wakiwakaribisha, vileni vyakula viwekwavyo mbele yenu. Waponyeni wagonjwa waliomo, waambieni, Ufalme wa Mungu umewakaribia.” (mstari wa 8,9).
Huu ndio ulikuwa uzito wa ujumbe wao. Hawakutakiwa kupoteza shabaha ya ujumbe huu kwa kuingia katika mabishano ya mambo yasiyo ya msingi ambayo yangefunga mlango wa kweli za muhimu walizoagizwa na Yesu kuwafundisha. Walitakiwa kufundisha kuanzia Agano la Kale wakielezea unabii wa utume na kazi ya Kristo, na kuuwasilisha ujumbe ambao utalainisha mioyo ya watu ili waweze kuandaliwa kumpokea Kristo, pindi atakapofuatia...
Hawa wanafunzi sabini hawakuwa kama wale kumi na wawili waliokuwa wakitembea na Yesu, lakini bado waliyasikia mafundisho na maelekezo ya Yesu mara kwa mara. Walitumwa chini ya maelekezo yake kufanya kazi kama Yeye alivyofanya. Mahali popote walipoenda walitakiwa kupeleka ujumbe wa, “ Ufalme wa Mungu umekuja kwenu, wote watakaoupokea ujumbe na mjumbe Wake wataingizwa katika ufalme wake. Hii ndiyo siku ya kujiliwa kwenu.” Walipaswa kuwasilisha kweli ya Mungu katika namna ambayo watu wangeongozwa kupata baraka walizowekewa.
—Letter 119, April 14, 1905,, to the members of the Nashville church.
Post a Comment