MWANA MITINDO TOYIN APEWA LAWAMA JUU YA MAVAZI YAKE
Mwanamitindo ya mavazi maarufu nchini Nigeria kwa jina Toyin Lawani, amekashifiwa na wengi mitandaoni nchini Nigeria hasa wale ambao ni waumini wa kanisa Katoliki.
Hii ni baada yake kuchapisha picha zake akiwa amevaa vazi maalum ambalo aliunda na kuvaa kwenye hafla ya uzinduzi wa filamu ya Nollywood ambayo inaitwa, “The Prophetess” ambapo alikuwa mmoja wa wageni waalikwa.
Vazi hilo linaigiza lile la watawa wa kanisa katoliki lakini limepasuliwa mara mbili mbele na kuacha mapaja yote nje.
Picha hizo za Toyin Lawani zimesambaa sana na wengi wanahisi kwamba aliikosea heshima kanisa Katoliki na hasa watawa na hata kuchukulia kitendo chake kuwa cha kukufuru.
Hata hivyo mwanadada huyo mmiliki wa kampuni ya “Tiana Place Empire” hatishwi na maneno ya watu kutokana na maneno ambayo anaendelea kusema kwenye akaunti ya kampuni yake ambapo anaendelea kuchapisha picha hizo.
Hii leo amechapisha video ambayo inaonyesha wakati alikuwa akipigwa picha za vazi hilo akisema yeye kama mungu wa kike wa mitindo ya mavazi haulizwi maswali na binadamu. Baadaye aliamkua wafuasi wake na kusifia vazi lake.
Post a Comment