AMKA NA BWANA LEO 13

KESHA LA ASUBUHI

Jumanne 13/04/2021

*YESU, MKATE WA UZIMA*

*Amin, amin, nawaambia, Yeye aaminiye yuna uzima wa milele. Mimi ndimi chakula cha uzima. Baba zenu waliila mana jangwani; wakafa. Hiki ni chakula kishukacho kutoka mbinguni, kwamba mtu akile wala asife. Mimi ndimi chakula chenye uzima kilichoshuka kutoka mbinguni; mtu akila chakula hiki, ataishi milele. Na chakula nitakachotoa mimi ni mwili wangu, kwa ajili ya uzima wa ulimwengu.* *Yohana 6:47—51*

 Swali liliulizwa, Tufanye nini ili tuweze kufanya kazi ya Mungu? Tufanye nini tuweze kuipata mbingu? swali hili la muhimu linajibiwa kwa wote wanaotamani kujua, "Hii ndiyo kazi ya Mungu, mmwamini yeye aliyetumwa na yeye"  (Yohana 6:29)... “Kwa maana chakula cha Mungu ni kile kishukacho kutoka mbinguni na kuupa ulimwengu uzima.” (mstari wa 33). “Mimi ndimi chakula cha uzima; yeye ajaye kwangu hataona njaa kabisa, naye aniaminiye hataona kiu kamwe.” (mstari wa 35). 

Kristo anawapa kuelewa kwamba mwanadamu anahitaji kufundishwa na Mungu ili kutambua mambo haya. Hii ni kazi ya ufahamu mrahisi zaidi wa maandiko katika kanisa la leo. Wachungaji wanahubiri kipengele tu cha Neno, na hawatendi kadiri wanavyofundisha. Hii inasababisha uelewa mbaya wa Neno na mafundisho, inatengeneza makosa na tafsiri tenge ya maandiko.

*Tunaweza kufundishwa na mwanadamu kuuona ukweli kwa bayana, Lakini Mungu pekee ndiye anayeweza kuufundisha moyo kupokea kwa jinsi ya wokovu, yaani kupokea maneno ya uzima wa milele kwa moyo mwema wa dhati. Bwana anangoja kwa uvumilivu kuielekeza kila nafsi iliyo tayari kufundishwa. *Tatizo halipo kwa Mkufunzi aliyepo tayari, Mwalimu mkuu ambaye ulimwengu umewahi kuwa naye, bali tatizo liko kwa mwanafunzi anayeshikilia fikra na mawazo yake, na hayuko tayari kusalimisha nadharia zake za kibinadamu na kuja kwa unyenyekevu kufundishwa*. Haruhusu dhamiri na moyo wake kuelemishwa, kunidhamishwa kufunzwa na kufanya kazi kama mkulima anayefanya kazi duniani na kama msanifu katika kujenga jengo.

*Kila mtu anahitaji kufanyiwa kazi, kufinyangwa na kutengenezwa kufanana na Mungu. Kristo anakuambia wewe rafiki yangu mpendwa, mdogo kwa mkubwa, ukweli wa milele “ Msipoula mwili wake Mwana wa Adamu na kuinywa damu yake, hamna uzima ndani yenu.” (mstari wa 53). Kama hautalichukulia Neno la Kristo kama mshauri wako, hautaweza kudhihirisha hekima yake au maisha Yake ya kiroho.*

*MUNGU ATUBARIKI TUNAPOTAFAKARI NENO LAKE*

No comments