AMKA NA BWANA LEO 15
KESHA LA ASUBUHI
Alhamisi 15/04/2021
*NITAKULINDA*
*Kwa kuwa umelishika neno la subira yangu, mimi nami nitakulinda, utoke katika saa ya kujaribiwa iliyo tayari kuujilia ulimwengu wote, kuwajaribu wakaao juu ya nchi.* *Ufunuo 3:10*
Haya maneno ni ya kweli na hakika, na litakuwa jambo la manufaa kwetu kuyachukua na kuchunguza maandiko ili kupata rejea ya maana yake halisi. *Saa ya kujaribiwa yaja juu ya ulimwengu wote, kuwajaribu wakaao juu ya nchi. Ingawa hatutaki kutengeneza wakati wa taabu kwa ajili yetu wala hatutamani kuugulia taabu ijayo, bado tunatakiwa kuunganika kwa karibu sana na Mungu ili tusianguke majaribuni pindi yajapo. *“Ni nani miongoni mwenu amchaye Bwana, aitiiye sauti ya mtumishi wake? Yeye aendaye katika giza, wala hana nuru, naye alitumainia jina la Bwana, na kumtegemea Mungu wake.” (Isaya 50:10)*
*Bwana atapambana kwa ajili yetu dhidi ya adui.* Tunatakiwa kuamini kuwa tunao msaada katika Mungu na kwamba hatutaogopa, wala hatutajawa na hofu na bumbuazi; Kwani tunajua kuwa Mungu wa Israeli amekuwa na watu wake tangu mwanzo kabisa —tangu kuanza kwa ulimwengu huu Mungu amekuwa pamoja na watoto wake watiifu. *Ni lazima tuoneshe kuwa tunao ujasiri kwa Mungu na tudhihirishe hilo kwa ulimwengu kwamba tunaweza kumtumainia kwa sababu tunamwamini. *Neno lake limeahidi kuwa hakuna jaribu litakalotujia, kwani msaada utatolewa kututegemeza.*
Tunategemea katika siku hizi za mwisho kuwa majaribu yatakuja; Hatutazamii kitu chochote kingine; bali Mungu atupatie neema ili kwamba tuweze kuyastahimili majaribu yajapo, na tusizimie katika mateso. Hatutamani kuwa mahali ambapo hatutakuwa na nguvu wakati huo. Kwa hiyo tuwe na uzoefu na Mungu sasa...
Mungu anao watu ambao hawatapokea alama ya mnyama katika mkono wao wa kuume wala katika vipaji vya nyuso zao. Mungu anayo sehemu kwa ajili ya watu wake kujaza katika ulimwengu huu, ili kuakisi nuru. Wewe ni mlinzi wa Mungu. Yesu anasema kuhusu watu wake, *“Ninyi ni nuru ya ulimwengu. Mji hauwezi kusitirika ukiwa juu ya mlima.” (Mathayo 5:14)*.
*Mungu aliifanya sheria Yake kwa ajili ya ulimwengu wote. Alimuumba mwanadamu, akitoa zawadi tele za asili, anashikilia pumzi yetu na maisha yetu mikononi mwake. Anatakiwa kutambuliwa, na sheria yake kuheshimiwa mbele ya watu wote wenye mamlaka ya kidunia.*
*TAFAKARI NJEMA MUNGU AKUBARIKI MPENDWA*
Post a Comment