AMKA NA BWANA LEO 16

KESHA LA ASUBUHI

Ijumaa 16/04/2021

*TOENI KWA KADIRI MLIVYOPOKEA*

*Mmepata bure, toeni bure.* *Mathayo 10:8* 

Vipaji visivyotarajiwa vitaendelezwa kwa watu wa maisha ya kawaida. Kama wanaume na wanawake watapata ujumbe wa kweli waliopewa, wengi watakaosikia wataupokea. Watu wa kila tabaka la maisha, tabaka la juu na la chini, matajiri na masikini wataukubali ujumbe wa leo. Baadhi wanaochukuliwa kama wasio na elimu wataitwa katika huduma ya Bwana, kama wavuvi wanyenyekevu wasio na elimu walivyoitwa na Mwokozi. Watu wataitwa wakiwa wameshikilia plau kama ilivyokuwa kwa Elisha, na watasukumwa kuchukua kazi ambayo Mungu amewaitia. *Wataanza kufanya kazi katika usahili na utulivu, wakisoma na kuyaelezea maandiko kwa wengine. Jitihada zao sahili zitafanikiwa.*

Kazi ya nyumba kwa nyumba itafanywa na wanaume na wanawake watakaotambua kuwa wanaweza kumfanyia kazi Bwana kwa sababu ameweka Roho yake juu yao. Kadri watakavyoenenda katika unyenyekevu wa imani Bwana atawapatia neema ambayo watawapatia watu wengine. *Bwana atawapatia upendo uleule kwa wanaopotea kama alivyowapatia wanafunzi wa awali,*

Katika siku zijazo wanadamu ambao kupitia kwao malaika wanaweza kutenda kazi wataukubali ukweli. Hapo zamani, malaika wa mbinguni walifanya kazi kwa kushirikiana na wakala wa kibinadamu, wakiwapatia nguvu ya lugha na nguvu ya ushawishi wa hoja ambazo zilifikia ngome za nafsi. Wafanya kazi wanaoonekana kama wasio wasomi, watu ambao hawakuelimika, mara nyingi wana mivuto ya ajabu kwa wema... 

Hakuna ambaye amepata miale kutoka katika Jua la Haki atakayekosa maneno yanayofaa. *Haitakuwa ufasaha wa kuhutubu kama ulimwengu unavyouchukulia, bali ni umbuji wa kimbingu. Watatamka maneno yatakayoenda moja kwa moja akilini na kuamsha uongofu na kuwafanya wasikilizaji wao waulize, Kweli ni nini?*

*Watendakazi wa aina hiyo tunaweza kuwatia moyo kwa kusema, Nina uhakika kuwa mtatoa ushawishi wa wema katika kazi hii kubwa na takatifu, kama mtajichunguza, mkitambua kuwa ninyi ni watii wa neema inayookoa, mlioletwa katika mahusiano ya familia takatifu na Mungu, kupitia Yesu Kristo na kutumwa kufanya kazi kwa ajili ya kuokoa roho.*

*MUNGU AKUBARIKI SANA MPENDWA*

No comments