FAHAMU ZAIDI, MFALME WA PORI JONAS SAVIMBI ALIYEISUMBUA SERIKALI YA ANGOLA KWA MIAKA 27

FAHAMUZAIDI:MFALME WA PORI JONAS SAVIMBI ALIYEISUMBUA SERIKALI YA ANGOLA KWA MIAKA 27

Februari 22, 2002 vyombo vingi vya habari duniani kote vilitawaliwa na habari kubwa ya kuuawa kwa "MFALME WA PORI" na mwanaume aliyeisumbua serikali ya Angola kwa zaidi ya miaka 27 akiongoza vita vya msituni dhidi ya vikosi vya serikali. 

"JONAS MALHEIRO SAVIMBI"  alikuwa mtoto wa pekee kwa baba yake (Lote), aliyekuwa mfanyakazi wa reli ya Benguela na mhubiri wa kanisa la Protestanti lililokuwa likifadhiliwa na Wamarekani.

Pamoja na baba yake kuwa muumini wa dini kamwe Jonas hakuwa muumini, na tangu utoto wake alikuwa ni mtukutu sana.

Alisoma katika shule za Kiprotestanti na Kikatoliki, lakini akiwa na miaka 24 alipata udhamini wa kwenda kusoma Ureno ambapo alimalizia masomo yake ya sekondari na somo la lazima la siasa huku akishindwa kuanza kwa wakati masomo ya udaktari wa binadamu aliyotakiwa kuyachukua.

Mwaka 1966 alianzisha vuguvugu la Unita kama harakati ya kukomboa Angola kutoka ukoloni wa Ureno.

Katika nyakati zake za awali, kabla ya kuanzisha Unita, alijiunga na chama cha wapigania uhuru wa MPLA mwaka 1964, muda mfupi baadaye alijiunga na chama cha FNLA. 

Mwaka huohuo alipata fursa ya kufanya ziara maalumu China na aliahidiwa kupatiwa nafasi zaidi kwa ajili ya mafunzo ya kijeshi na misaada ya zana za kijeshi.

Hatua hiyo ilitokana na mgongano wa kimasilahi, baada ya FNLA na MPLA kuanza kupingana kuhusu nani anastahili kupewa .nchi iwapo watapata uhuru, hivyo muda mfupi baadaye wakoloni hao walitoa taarifa kueleza kwamba Savimbi anapigana kwa ajili ya masilahi yao.

Hatua hiyo ilisababisha kuungwa mkono na Marekani iliyokuwa na masilahi tofauti na MPLA iliyoungwa mkono na Wasovieti tangu mwaka 1974 na kilijipambanua kufuata mrengo wa Marxist-Leninst kuanzia mwaka 1977, wakati Savimbi alijipambanua kufuata sera za Mao na kuungwa mkono na China.

Vita baina ya MPLA na Unita hata hivyo ilikuwa na sababu nyingi za ndani na kwa hiyo kuanza kutumiwa kama chanzo cha mvutano wakati wa vita baridi baina ya Marekani na USSR.

No comments