CEO SENZO MAZINGISA: UZOEFU WA KOCHA MPYA WA YANGA UTASAIDIA SANA KLABU YA YANGA

Mshauri wa Masuala ya Mabadiliko ndani ya Klabu ya Yanga Senzo Mazingisa amesema uzoefu wa kocha mpya wa Yanga utaisaidia sana klabu ya Yanga

"Huyu ni kocha mzuri sana, kafundisha Congo, Sudan na timu nyingine pia ana makombe mengi ndani ya timu nyingi ambazo amezifundisha, hivyo tunaamini uzoefu mzuri alionao utatusaidia sana"

“Kwa klabu kama Yanga tumefurahi kumpata kocha kama huyu, kama ambavyo mmeona tulikuwa na presha ya makocha waliopita kulingana uhitaji wa timu, tunatarajia kupata kilicho bora kutoka kwa kocha huyu mpya,” alisema Mazingiaa

No comments