AMKA NA BWANA LEO 9
KESHA LA ASUBUHI
IJUMAA, APRILI, 9, 2021
SOMO: KUISHI MAISHA MAPYA
Basi yo yote myatakayo mtendewe na watu, nanyi watendeeni vivyo hivyo; maana hiyo ndiyo torati na manabii.
Mathayo 7:12
Kristo alikuja kutufundisha siyo tu yale tupaswayo kuyafahamu na kuyaamini, bali pia yale tunayopaswa kuyatenda katika mahusiano yetu na Mungu pamoja na wanadamu wenzetu. Kanuni ya msingi ya usawa inatutaka tuwafanyie wengine kama vile ambavyo wangetutendea. Tunatakiwa daima kukumbuka maslahi yao ya milele, tukijiambia “Wamenunuliwa kwa damu ya thamani ya Mwokozi.”
Katika kushughulika kwetu kote na wanadamu wenzetu, wawe waumini au wasio waumini, tunatakiwa kuwatendea kama ambavyo Kristo angewatendea akiwa katika nafasi yetu. Kama tunatii sheria za Mungu kwa mema yetu ya sasa na ya umilele itakuwa ni kwa mema yao ya sasa naya milele nao kuzitii. Lengo letu kuu ni kuwa watendakazi wa huduma za kimishenari kwa njia ya tiba sawasawa na maelekezo ya Kristo ...
Wote watakaoingia katika mji wa Mungu kupitia malango ya lulu lazima wawe wamemtanguliza Kristo katika mambo yao yote. Ni hili litakalowafanya wajumbe wa Kristo, mashahidi Wake. Watabeba ushuhuda wa wazi dhidi ya matendo yote maovu, wakiwaelekeza kwa Mwanakondoo wa Mungu achukuaye dhambi za ulimwengu. Wote wanaompokea Yeye anawapatia, nguvu ya kuwa wana wa Mungu.
Uongofu ni njia pekee ambayo kwayo tunaweza kuufikia mji mtakatifu. Mlango tunaouingia ni mwembamba na mnyoofu lakini katikati yake tunatakiwa kuwaongoza wanaume na wanawake na watoto kwa kuwafundisha kwamba ili waweze kuokolewa ni lazima wawe na moyo mpya na roho mpya. Tabia za awali za kurithi zinatakiwa kushindwa. Matamanio ya asili ya moyo lazima yabadilishwe. Udanganyifu wote, uongo na kuongea maovu lazima viwekwe kando. Wanatakiwa kuishi maisha mapya yanayowafanya kuwa wanaume na wanawake wanaofanana na Kristo. Tunatakiwa kama ilivyokuwa, kuogelea dhidi ya mawimbi ya uovu.
Njia ya kwenda mbinguni ni nyembamba imezungushwa ua na sheria takatifu ya Yehova. Wale wanaoifuata njia hii kila mara ni lazima waikane nafsi. Ni lazima watii mafundisho ya Kristo... Hebu tusimtumaini mwanadamu bali tumtumaini Yesu Kristo aliyekufa ili kwamba atupatie haki.
—Letter 103, April 9, 1905,, to E. S. Ballenger, an administrator at the Paradise Valley Sanitarium.
Post a Comment