BINTI,MAHUSIANO NA MUNGU
KILA MWANAUME UNAMPENDA NA KUPOKEA VITU VYAKE, NI YUPI UTAISHI NAE KAMA MUME WAKO!??.
Wagalatia 6:7
"Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa cho chote apandacho mtu, ndicho atakachovuna"
Kuna wakati ndugu yangu unaweza kuishi maisha ukajiona mwenye bahati kubwa Sana maana kila unapopita wadhamini hujitokeza kutoa ofa kama sehemu ya ushawishi wa kuingizwa katika mahusiano ya kimkakati.
Kila anayekuja mbele yako anakuja akitanguliza vitu ili kuonyesha namna alivyo mtu wa kukujali na kukuthamini bila kufahamu nyuma ya vitu hivyo Kuna mkakati upi.
Mpokeaji unapokea kwa furaha kubwa ukiamini kuwa ni mwaka wa bahati na mafanikio maana Mungu amekuletea wahisani ambao watakuvusha kutoka ulipo bila kujua kitu gani kinatafutwa ndani yako.
Mwanamke/Binti tambua kila jambo/kitu kinacholetwa kwako Kama sehemu ya ushawishi wa kuingizwa mahusiano; Hubeba mkakati mkubwa wa Siri ambao lengo ni kumpoteza mpokeaji ambae anawindwa bila kufahamu kuwa anawindwa.
Sio kweli kuwa vitu unavyopewa/unavyokea vinadhihirisha maana halisi ya Upendo. Upendo wa kweli umetulia unadhihirishwa na nia dhabiti ya kumwelekea MUNGU. Upendo wowote usio thibitisha uhalisia wa uwepo wa Mungu ni uongo.
Swali la msingi la kujiuliza ni kuwa, ikiwa kila anayekuja mbele yako na kukueleza kuwa anakupenda na kukupa vita na wewe unavipokea, je utaishi na nani kwa mfumo wa Namna hiyo?
Madhara makubwa ya kupokea vitu ovyo ovyo ni kujengewa Ufahamu wa utegemezi na kuishi kwa kutegemea wahisani. Ikiwa wahisani watatoweka Ni wazi utaishi Maisha ya kuendelea kujirahisisha kwa wanaume ili upate msaada wa kuishi.
Usijengee mazingira ya kupokea vitu kutoka kwa wanaume, bali jiwekee mazingira ya kutunza heshima yako ili vitu visiharibu thamani na Heshima yako. Heshima yako itajengwa kwa nidhamu ambayo utaiweka katika Maisha yako.
Tabia ya vitu hupofusha Akili, Fikra, Mawazo na mtazamo wa mtu. Nidhamu na Heshima huleta Hali ya kutunza misingi iliyojengwa katika kumpendeza Mungu na sio vinginevyo.
Jitunze bila kutegemea wahisani, Bali ishi kwa kumtegemea MUNGU katika mfumo mzima wa maisha yako.
ASANTE.
The Light Of Universe Ministry
Mwl Ejide Andrew Noah
+255743154575.
Post a Comment