tcra yamdaka anayetuhumiwa kusambaza stempu feki za kielektroniki

Mamlaka ya Mapato nchini Tanzania(TRA) Mkoa wa Kilimanjaro, imemkamata Mfanyabiashara maarufu Mjini Moshi aliyetambulika kwa jina moja la Mr Kimario kwa kujihusisha na mtandao wa kutengeneza na kusambaza stempu feki za kielektroniki (ETS) zenye jina la mamlaka hiyo wanazozibandikwa kwenye vinywaji feki.

Akizungumzia kukamatwa kwa Mfanyabiashara huyo, Meneja wa TRA Mkoani hapa, Gabriel Mwangosi alisema mfanyabiashara huyo alikamatwa juzi nyumbani kwake akiwa na shehena ya stempu hizo na kwamba, amekuwa akiuza stempu 100 kwa Sh10,000 na wakati mwingine hupunguza hadi Sh8,000.


"akuna ubishi kwamba kukua kwa uchumi wa nchi yetu ungekuwa kwa kiwango cha juu zaidi kama kungekuwa hakuna watu wanatuhujumu kwa utaratibu huu, athari yake ni kubwa kwa uchumi wa nchi lakini kutoa vinywaji visivyofaa vikahalalishwa,"alisema Kundya

"Mapato yaliyosatahili kuingia kwenye mfumo rasmi wa serikali yakahujumiwa kwa utaratibu huu yanakwenda kwa watu ambao hawakustahili na kuisababishia serikali hasara," alisema Kundya

Kundya alisema uharamu wa biashara hiyo ni hatari kwa maisha ya watu na uchumi wa Taifa na kwamba serikali haitavumilia vitendo hivyo vinaendelea kwenye jamii kwasababu ni uhujumu uchumi.

"Lazima mapambano yaendelee kwa nguvu zote ili kuhakikisha kwamba jamii yetu inapata maendeleo yaliyokusudiwa na serikali yetu,” alisema Kundya.

Itakumbukwa, aliyewahi kuwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Stella Manyanya akizungumza jijini Dodoma Septemba 16, 2019, alisema tatizo la bidhaa bandia nchini limepungua kwa kiasi kikubwa kutokana na matumizi ya stempu za kielekroniki  (ETS).

Serikali ilitangaza kuanza kutumia mfumo wa ETS katika kukusanya kodi mwaka wa fedha 2018/19, lengo likiwa ni kudhibiti udanganyifu wa wazalishaji wa bidhaa zinazotozwa ushuru wa bidhaa.

Awamu ya kwanza ya mfumo wa ETS ulianza rasmi Januari 15 mwaka huu (2019) ambapo stempu za kielektroniki zilianza kubandikwa katika bidhaa 19 za aina ya vilevi tofauti tofauti.

Awamu ya pili ilianza Agosti 1, 2019 ikihusisha bidhaa za vinywaji baridi.

Kwa mujibu wa Manyanya, mbali na kusaidia Serikali kuongeza makusanyo ya kodi, lakini pia matumizi ya stempu hizo yalisaidia kupunguza tatizo la bidhaa bandia sokoni.

Akizungumza Jijini Dodoma Machi 11, 2020, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Phillip Mpango alipokuwa akiwasilisha mapendekezo ya Serikali ya mpango wa maendeleo wa Taifa na ya kiwango na ukomo wa Bajeti kwa mwaka wa fedha 2020/2021, alisema pamoja na mafanikio makubwa yaliyopatikana katika ukusanyaji wa mapato ya kodi kwa kipindi kile,  Serikali iliahidi kuendelea kuhimiza matumizi ya ETS, ili kuwadhibiti wale wanaokwepa kulipa kodi.

Waziri huyo alisema lengo la kufanya hivyo ni kutaka kuendelea kusimamia matumizi ya stempu hizo katika bidhaa zinazotozwa ushuru wa bidhaa na kupitia nyaraka za walipakodi.

lisema tangu kuanza kwa matumizi yake kupitia kwa nyaraka za walipakodi, lengo la kufanya usuluhishi wa kodi walizolipa kwa kujikadiria wao wenyewe lilikuwa likitekelezeka  kwa kulinganisha na kiasi halisi walichopaswa kulipa kwa mujibu wa Sheria.

Pia, alisema Serikali ilikuwa ikichukua hatua mbalimbali za kuongeza makusanyo zaidi na miongoni mwa hatua hizo ni pamoja na kuendelea kusimamia utekelezaji wa sheria, kanuni na taratibu za kodi na kuhakikisha mfumo wa usimamizi wa mashine za kielektroniki za kutolea risiti unatumika ipasavyo.

Kwa maana nyingine, “tutaendelea na utoaji wa elimu kwa mlipakodi na dhana ya ‘ukinunua dai risiti na ukiuza toa risiti.’


No comments