Mwandishi wa habari aliyefukuzwa kazi baada ya kukososa mahojiano ya Harry na Meghan asema hajuti

Piers Morgan amesema kuwa hakwepi ukosaji wake wa Mwanamfalme Harry na Meghan alioutoa kwenye kipindi cha televisheni ya ITV nchini Uingereza maarufu kama-Good Morning Britain mara ya kwanza kwenda hewani baada ya kuondoka kwake.

Ilitangazwa kuwa Bw Morgan ambaye alikuwa ndiye mtangazaji wa kipindi hicho maarufu aliacha kazi ya utangazaji wa kipindi hicho baada ya kusema "hakuamini hata neno moja " alilosema Meghan katika mahojiano na Oprah Winfrey.

Akielezea kuondoka kwake, mtangazaji mwenza Susanna Reid alisema kuwa alisema kuwa hakubaliani na kauli zake, na kuongeza kuwa: "Kipindi kinaendelea."

Ofcom inapeleleza kauli zake baada ya kupokea malalamiko 41,000.

Katika ujumbe wake wa Twitter alioutuma wakati kipindi kilipokuwa kinaanza, Morgan alisema: "Jumatatu, nilisema sikumuani Meghan Markle katika mahojiano yake ya Oprah. Nimekuwa na muda wa kutathmini maoni haya, na bado nasema simuamini."

Aliongeza kuwa: "Uhuru wa kujieleza ni mlima ninafurahi kufa juu yake. Asante kwa upendo wote na chuki. Ninaondoka kuishi kwa muda na maoni yangu."

Ujumbe wake uliambatana na picha ya Winston Churchill wenye nukuu kuhusu uhuru wa kujieleza.

Jumanne, kabla ya kuondoka kwenye kipindi, Morgan aliibua malumbano baada ya mjadala na mtangazaji mwenzake Alex Beresford kuwahusu Mwanamfalme Harry na mkewe Meghan.

Piers Morgan alisema nini kingine?

Akizungumza kutoka mbele ya nyumbani kwake mjini London Jumatano, mtangazaji huyo alielezea kuondoka kwake kwenye kituo cha ITV kama "faraja", akiongeza kuwa : "Nilikuwa na mazungumzo mazuri na ITV na tulikubaliana kutoafikiana ."

Alifafaniua: "Ninaamini katika uhuru wa kujieleza, ninaamini katika haki ya kuruhusiwa kuwa na maoni.

Kama watu wanataka kumuamini Meghan Markle, ni haki yao.

"Siamini karibu kila kitu kilichotoka mdomoni mwaka na ninadhani uharibufu alioufanya kwa Ufalme wa Uingereza na Malkia katika wakati ambapo Mwanamfalme Philip amelazwa hospitalini ni mkubwa na wa kudharauliwa kusema kweli.

"Kama itabidi nichukie simu yangu kwa kujieleza maoni yangu kumuhusu Meghan Markle na machungu yake aliyoyatoa kwenye mahojiano, basi na iwe hivyo."

Pia alisema kuwa: "Ninadhani ni haki kusema, ingawa watu wengi watafikiria kuwa wamenifuta mimi, ninadhani badala yake wataka tamaa wakati nitakaporejea tena ."

Ameelezea kutoonekana kwake katika televisheni kwa siku zijazo kama "kwa muda tu", akiongeza kuwa "wakati wote hufanya mazungumzo na watu " kuhusu kazi .

No comments