SIKU ZA MWISHO
🤔🤔
*je, ni matukio gani yatatukia YESU ajapo mala ya pili??*
🤔🤔
Watu wengi wamedhani kuwa watu wa MUNGU watapotea tu wakitumia fungu hili
👇👇
Mathayo 24:40-42
[40]Wakati ule watu wawili watakuwako kondeni; mmoja atwaliwa, mmoja aachwa;
[41]wanawake wawili watakuwa wakisaga; mmoja atwaliwa, mmoja aachwa.
[42]Kesheni basi; kwa maana hamjui ni siku ipi atakayokuja Bwana wenu.
👆👆
fungu hili lilikuwa unabii wa kufungwa kwa mlango wa rehema ambapo ukisoma Ufunuo wa Yohana 22:11
[11]Mwenye kudhulumu na azidi kudhulumu; na mwenye uchafu na azidi kuwa mchafu; na mwenye haki na azidi kufanya haki; na mtakatifu na azidi kutakaswa.
👆👆
Hivyo hapo ndipo itaamriwa kua yupi ataenda jehanam na yupi ataingia mbinguni maana rehema itakuwa imekoma na hakuna maombezi tena. Kwa ufupi kuhusu ujio wa YESU tazama hii
👇
*https://youtu.be/0xYxD6Gj1jM*
👆👆
1. WALIOKUFA WAKIWA SAFI KTK IMANI YA KRISTO WATAFUFULIWA KWANZA:
"Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza."
1 Wathesalonike 4:16
" ........maana parapanda italia, na wafu watafufuliwa,.... 1 Wakorintho 15:52
2. WALIO HAI NA WAKIWA SAFI KTK IMANI YA KRISTO WATABADILISHWA NA KUVAA MWILI WA KUTOKUFA, NAO WATAUNGANA NA WATAKATIFU WALIOFUFUKA, WATACHUKULIWA NA YESU KWENDA NAO MBINGUNI.
" Angalieni, nawaambia ninyi siri; hatutalala sote, lakini sote tutabadilika,.... Maana sharti huu uharibikao uvae kutokuharibika, nao huu wa kufa uvae kutokufa. 1 Wakorintho 15:51-53
"Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele." 1 Wathesalonike 4:17
3. WAOVU WATAKAOKUTWA HAI WATAKUFA WATAKAPOUONA UTUKUFU WA YESU, WATAUNGANA KTK MAUTI NA WAOVU WENZAO WALIOTANGULIA KUFA, UFUFUO WAO BADO, HUU UFUFUO WA KWANZA NI WA WATAKATIFU TU.
"Hao wafu waliosalia hawakuwa hai, hata itimie ile miaka elfu. Huo ndio ufufuo wa kwanza. Heri, na mtakatifu, ni yeye aliye na sehemu katika ufufuo wa kwanza; juu ya hao mauti ya pili haina nguvu; bali watakuwa makuhani wa Mungu na wa Kristo, nao watatawala pamoja naye hiyo miaka elfu." Ufunuo 20:5,6
5. SHETANI ATATIWA KTK KIFUNGO (KUZIMU), MAANA YAKE NI HATOKUWA NA MTU WA KUMDANGANYA HAPA DUNIANI. ATABAKI YEYE NA MALAIKA ZAKE TU (MAPEPO/MAJINI)
" Akamshika yule joka, yule nyoka wa zamani, ambaye ni Ibilisi na Shetani, akamfunga miaka elfu; akamtupa katika kuzimu, akamfunga, akatia muhuri juu yake, asipate kuwadanganya mataifa tena, hata ile miaka elfu itimie; na baada ya hayo yapasa afunguliwe muda mchache." Ufunuo 20:2,3
6. BAADA YA MIAKA ELFU KWISHA, YESU, WATAKATIFU NA YERUSALEMU MPYA WATASHUKA. HAPO WAFU WAOVU WATAFUFULIWA (UFUFUO WA PILI), NA KUFUFULIWA KWAO NDIO KUFUNGULIWA KWA SHETANI TOKA KIFUNGONI, NA ANAANZA KAZI YAKE TENA.
" Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake; na Mauti na Kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake...." Ufunuo 20:13
WANAFUFULIWA ILI WAPATE HUKUMU KISHA WAFE TENA MAUTI YA PILI.
" Mauti na Kuzimu zikatupwa katika lile ziwa la moto. Hii ndiyo mauti ya pili, yaani, hilo ziwa la moto. Na iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto. Ufunuo 20:14,15
7. BAADA YA MOTO KUUNGUZA DHAMBI NA MDHAMBI NA KUTEKETEZA KABISA, NDIPO MBINGU MPYA NA NCHI MPYA ZITAKAPOSHUKA NA KUTULIA JUU YA DUNIA HII AMBAYO ITAKUWA IMETAKASWA KWA HUO MOTO.
" Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya; kwa maana mbingu za kwanza na nchi ya kwanza zimekwisha kupita, wala hapana bahari tena. Nami nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, umewekwa tayari, kama bibi-arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe. Nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atafanya maskani yake pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao. Ufunuo 21:1-3
8. BAADA YA MBINGU MPYA NA NCHI MPYA KUKAA MAHALI PAKE, MAISHA YASIYO YA DHAMBI YATAENDELEA. YOTE MENGINE YA DUNIANI YATAKUWA YAMEPITA ISIPOKUWA SABATO ITADUMU HATA KTK MBINGU MPYA NA NCHI MPYA.
"Kama vile mbingu mpya na nchi mpya, nitakazofanya, zitakavyokaa mbele zangu, asema BWANA, ndivyo uzao wenu na jina lenu litakavyokaa.
Na itakuwa, mwezi mpya hata mwezi mpya, na sabato hata sabato, wanadamu wote watakuja kuabudu mbele zangu, asema BWANA.
Nao watatoka nje na kuitazama mizoga ya watu walioniasi; maana funza wao hatakufa, wala moto wao hautazimika nao watakuwa chukizo machoni pa wote wenye mwili." ISAYA 66:22-24
9. Baada ya kufanya ibada ya kukusanyika mbele za MUNGU kila sabato na mwezi mpya tutatoka nje na kucheza cheza tukiwakanyaga waovu walio majivu ambao watakuwa majivu. *hivyo ibada ya kumuabudu MUNGU wetu haitakuwa siku zote bali itakua ya kila sabato na kila mwezi mpya*
Malaki 4:1-3
[1]Kwa maana, angalieni, siku ile inakuja, inawaka kama tanuru; na watu wote wenye kiburi, nao wote watendao uovu, watakuwa makapi; na siku ile inayokuja itawateketeza, asema BWANA wa majeshi; hata haitawaachia shina wala tawi.
[2]Lakini kwenu ninyi mnaolicha jina langu, jua la haki litawazukia, lenye kuponya katika mbawa zake; nanyi mtatoka nje, na kucheza-cheza kama ndama wa mazizini.
[3]Nanyi mtawakanyaga waovu; maana watakuwa majivu chini ya nyayo za miguu yenu; katika siku ile niifanyayo, asema BWANA wa majeshi.
Mungu awabariki tunapojiandaa kumpokea Yesu ajapo.
🙏🙏
*TAFADHALI SAMBAZA KWA WENGINE* 🙏🙏
Ubalikiwe nimepata kuelewa juu ya aina ya ufufuo
ReplyDelete