AMKA NA BWANA LEO 28
KESHA LA ASUBUHI
JUMAPILI, MACHI, 28, 2021
SOMO: UWEPO WAKE UNAODUMU
Utanijulisha njia ya uzima; mbele za uso wako ziko furaha tele; na katika mkono wako wa kuume mna mema ya milele.
Zaburi 16:11.
Ulimwengu huu ni shule yetu —shule ya nidhamu na kujifunza. Tumewekwa hapa kutengeneza tabia kama tabia ya Kristo, na kupata mienendo na lugha ya maisha ya juu. Mivuto inayopinga mema, imejaa kila upande. Maendeleo ya dhambi yanazidi kuongezeka, ya kina sana, ya kuchukiza sana kwa Mungu, kwamba muda si mrefu atainuka katika ukuu wake kuitikisa dunia ajabu.
Mipango ya adui ni ya hila sana, utata anaouleta ni wa hadaa sana, kiasi kwamba wale walio dhaifu katika imani hawawezi kuyatambua madanganyo yake. Wanaanguka katika mitego iliyoandaliwa na Shetani, anayetenda kazi kupitia wakala wa kibinadamu kudanganya kama yumkini hata walio wateule. Wale tu waliounganishwa kwa karibu na Mungu wataweza kutambua madanganyo, njama, za adui....
Fikiri kuhusu utukufu unaowangoja wanaoshinda! Watauona uso wake yeye ambaye katika uwepo wake kuna ukamilifu wa furaha na ambaye katika mkono wa kuume kuna raha milele. Hebu tumrusu Mungu kutawala fikra zetu. Hebu tusiseme au kutenda jambo lolote litakalomgeuza mwenzetu toka katika njia ya kwelli.
Ninahisi huzuni sana ninapowaza juu ya kiasi gani wachache hapo wanaoonesha kwamba wameonja baraka ya kina ya ushirika na Mwokozi aliyefufuka na kupaa. Watu wa dunia wanapambana kwa ajili ya ukuu. Wafuasi wa Mungu wanapaswa kumtazama Kristo kwa kudumu, wakiuliza, Hii ndiyo njia ya Bwana? Tamanio takatifu ya kuishi maisha ya Kristo ijaze mioyo yetu. Ndani yake kuna ukamilifu wote wa Uungu katika mwili. Ndani yake zimefichwa hazina za hekima na maarifa.
Kwamba watu wetu waweze kutambua manufaa wanayoweza kuyapata ikiwa watadumu kumtazama Yesu. “Lakini sisi sote, kwa uso usiotiwa utaji, tukiurudisha utukufu wa Bwana, kama vile katika kioo, tunabadilishwa tufanane na mfano uo huo, toka utukufu hata utukufu, kama vile kwa utukufu utokao kwa Bwana, aliye Roho” (2 Wakorintho 3:18). Yeye ni Alfa na Omega wetu. Kukaza mwendo karibu naye na kudumisha ushirika naye, tunafanana naye. Kupitia kwa uwezo unaobadilisha wa Roho ya Kristo, tunabadilishwa katika moyo na maisha. Maneno yake yanaandikwa katika mbao za moyo, nasi ni mashahidi wake, tukimwakilisha katika maisha ya kila siku.
Post a Comment