mafunzo ya watu wazima leo 26

LESONI, MACHI 26

JIFUNZE ZAIDI:



Kuhusu utakaswaji wa mwisho wa Sayari Dunia dhidi ya dhambi, soma “Mwisho wa Pambano,” katika Pambano Kuu, uk. 384, 385 (Ellen G. White, The Great Controversy, uk. 662—678). 



“Kadiri miaka ya umilele inavyokwenda, ndivyo ufunuo wa utukufu wa Mungu na Kristo utakavyofunuliwa kwa ajabu. Kwa kadri watu watakavyojifunza tabia ya Mungu ndivyo watazidi kumwabudu na kumpenda. Kadiri Yesu anavyowafunulia siri za ukombozi wa vita kuu kati ya wema na ubaya ulioletwa na Shetani, ndivyo watakavyozidi kumtukuza na kumtumikia, na kumwimbia kwa sauti za watu maelfu mara maelfu makumi. 



'Na kila kiumbe kilichoko mbinguni na juu ya nchi na chini ya nchi ya juu ya bahari, na vitu vyote vilivyomo ndani yake, nalivisikia, vikisema, Baraka na heshima na utukufu na uweza una yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na yeye Mwana-Kondoo, hata milele na milele.” Ufunuo 5:13. 



“Mapambano makuu yamekoma. Dhambi na wenye dhambi hakuna tena. Ulimwengu mzima sasa umesafika. Umoja na ushirikiano ulio kamili kabisa umeenea ulimwenguni. Kutoka kwa Muumbaji hufurika uzima, nuru, na furaha na kuenea mahali pote. Tangu kitu kidogo mno mpaka kwa kikubwa kilinganacho na ulimwengu mzima, vitu vyote, vilivyo hai na visivyo hai, katika hali yao vyote, hutangaza kuwa Mungu ni pendo” —Ellen G. White, The Great Controversy, uk. 678.



MASWALI YA KUJADILI:

1. Kwa nini ahadi ya uzima wa milele katika mbingu mpya na nchi mpya ni ya msingi katika mafundisho yetu ya imani ya Kikristo? Pasipo ahadi hiyo imani yetu ingalikuwa batili jinsi gani? 



2. Soma 2 Petro 3:10—14. Ni kwa jinsi gani aya hizi huakisi wazo lililogusiwa katika Isaya 66? 


   Muhtasari: Isaya anatoa njozi yenye upeo mpana wa juu mno. Siyo tu kwamba Mungu atawasafisha na kuwarejesha upya watu wake wamwaminio, ila atatanua mipaka kuhusisha mataifa yote. Mwisho wa yote, uumbaji upya wa jumuia yake ya waaminio utaongoza kwenye uumbaji upya wa dunia, ambapo uwepo wake utakuwa faraja kuu kwa watu wake. 

No comments