amka na bwana leo 27
KESHA LA ASUBUHI
JUMAMOSI, MACHI, 27, 2021
SOMO: TULIA NDANI YA WOKOVU
Hatimaye, mzidi kuwa Hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake.
Waefeso 6:10.
Ikiwa mmeunganishwa kwa karibu na Yesu Kristo, Chanzo cha nuru na hekima, mnaweza kuwa wanaume na wanawake ndani ya Kristo. Tuna hiari sana kuridhika pasipo udhihirisho wowote wa kipekee wa ukaribu wetu na Mungu kiasi cha kushindwa ambapo tungefanikiwa. Kila hitaji limetolewa na Yesu kwamba tusije kuamini tu ukweli usiopendwa na wengi bali kwamba tuweze kuwa na furaha ndani yake. Kweli hutenda kazi katika upendo na imani hutenda kazi kwa upendo, na huitakasa nafsi....
Sasa swali ni, Je, unaupata ujuzi wa kweli? Unao muunganiko hai na Yesu Kristo? Unaona Ibrahimu alikuwa nao, na alizungumza na malaika, na angeweza kuwaomba hisani. Unaona Musa alikuwa na muunganiko hai na Mungu, na ombi lake la dhati lilikuwa aweze kuuona utukufu wa Mungu. “Nioneshe utukufu wako,” lilikuwa ombi lake. Hata hivyo, Bwana hakumkemea kwa kufanya hilo ombi; hakuwa mwenye kiburi katika kujaribu kufahamu mengi kumhusu Mungu na utukufu wake. Lakini tunaona kwamba yule mtu mkuu wa imani alifichwa katika ufa wa mwamba, na mkono wa Mungu uliwekwa juu ya mwamba, na kisha akamfunulia utukufu wake.
Hatuna udhati wa kutosha katika imani yetu au katika uzoefu wetu.... Niamini kuwa hakuna hata mmoja ambaye atatulia na nafasi ya mashindano kwa sababu mnaiamini kweli. Kama kungalipo na roho ya kuokoa katika dunia yote mnataka kujikaza wenyewe katika chanzo cha nuru yote na uweza kwamba mweze kuokoa hizi roho. Hamjali kuwa na tabia ya kidunia katika uzoefu wenu. Mnazo roho za kuokoa au kupoteza na mnahitaji mpango mkubwa zaidi wa Yesu kuletwa katika maisha yenu, katika tabia yenu, na katika uzoefu wenu. Mnaweza kuwa msaada na baraka ninyi kwa ninyi kwa kuwa waaminifu katika kila nafasi uliopo, kwa kuhisi kwamba wewe ni mwakilishi wa Mungu duniani....
Msiruhusu kweli, kwa kuwa inarudiwa mara nyingi kwenu, kuwa Swala lisilo na manufaa ya kipekee; lakini tuiruhusu itufae siku kwa siku kwa ajili ya kuwa katika jamii ya malaika wa mbinguni katika ufalme wa Mungu.
Post a Comment