mafunzo ya watu wazima leo 10

LESONI, MACHI 10

SOMO: MAPAMBANO YA MFUNGO (ISA. 58: 1—12) 



Siku kumi baada ya milio ya tarumbeta kuwakumbusha watu wa Mungu kwamba Bwana anahimidiwa kama Mfalme wao katika Siku ile hasa ya Upatanisho pale ambapo unyenyekevu wao kupitia kwa kujikana nafsi kunapaswa kuthibitisha uaminifu wao Kwake kama Mfalme, nabii huyo anainua sauti yake kama tarumbeta kutangaza kwamba wanamwasi (Isaya 58: 1). 



Soma Isaya 58:6—12. Ni matendo gani ambayo Mungu huyachukulia kuwa ni matendo halisi ya kujikana nafsi? Hata hivyo, ni lipi gumu zaidi, kuruka milo kadhaa au kutumia muda na pesa zako mwenyewe kuwalisha wasio na makazi katika mji wako? Ni Kanuni gani inaonekana kusababisha vitendo hivi? Je ni kwa jinsi gani vitendo hivi vinabeba ndani yake dini ya kweli?



Mtu yeyote anaweza kuwa mtu wa dini; mtu yeyote anaweza kupitia kaida za kidini, hata kaida zilizo sahihi, kwa wakati unaofaa, na kanuni zote sahihi. Lakini hiyo sio peke yake kile Bwana anachokitaka. Angalia maisha ya Yesu. Hata kama alikuwa mwaminifu kwa kaida za kidini za wakati Wake, waandishi wa injili walilenga zaidi matendo Yake ya rehema, uponyaji, kulisha, na msamaha kwa wale waliokuwa na mahitaji kuliko uaminifu wake kwa kaida. 



Bwana anatafuta kanisa, watu, ambao watahubiri ukweli kwa ulimwengu. Lakini ni nini kitakachovutia watu kwenye ukweli kama ulivyo katika Yesu: kufuata hasahasa sheria za lishe au utayari wa kusaidia wenye njaa? Kupumzika kabisa siku ya Sabato au utayari wa kutumia muda wako na nguvu zako kuwasaidia wale ambao wanahitaji? 



Soma Mathayo 25:40 na Yakobo 1:27. Yanatuambia nini?

Angalia baraka katika Isaya 58 ambazo Mungu anasema zitawajia wale wanaotafuta kuhudumia wale walio na hali duni. 



Unadhani Bwana anasema nini kwetu hapa? Je ahadi hizi za uingiliaji kati wa kimwujiza zinakuwapo katika maisha yetu pale tunapofanya mambo haya? Au, huenda, anatuambia juu ya baraka za kawaida tunazopokea kwa kujitoa wenyewe kwa wengine kinyume na tunapokuwa wabinafsi, walafi, na wenye kujipenda wenyewe? Elezea jibu lako. 

No comments