amka na Bwana
KESHA LA ASUBUHI
Jumatano 10/03/2021
*UTAWALA WA HAKI*
*Basi, Mungu wa amani aliyemleta tena kwa wafu...yeye Bwana wetu Yesu, awafanye ninyi kuwa wakamilifu katika kila tendo jema, mpate kufanya mapenzi yake; naye akifanya ndani yetu lipendezalo mbele zake, kwa Yesu Kristo.* *Waebrania 13:20, 21*
Mnapokuja pamoja kwa ajili ya ibada na kumtafuta Bwana, yapasa uwe na moja la kumpa heshima Yeye ambaye matakwa yake yote ni sawa na haki. Mapenzi Yake, yaliyotangazwa katika Neno Lake, yanapaswa yatekelezwe katika waraka. Utawala wa haki unaofunuliwa katika maisha ya watu wake wanaomkiri yapaswa kuwafanya wawe wenye mvuto. Tunapaswa kuishi kwa kuutazama daima utukufu wa Mungu, daima tukitafuta kuwa Wakristo katika kila maana ya neno.
Maneno haya yalisemwa na Mwalimu wetu: “Ninyi mnapaswa kuwa chini ya udhibiti wa Mungu. *Jifunzeni namna ya kupatana. Pendeni kama ndugu; iweni na huruma; kuweni wenye heshima*. Amri za Mungu ni za haki na sawa. Watenda kazi wake wote wanapaswa kuheshimiwa kama watenda kazi pamoja na Mungu.
Mivuto mbalimbali ya kazi yapasa ijengwe kwa uangalifu. Tangu wakati huu na kuendelea majukumu yataongezeka kwa haraka. Mapenzi ya Mungu, utawala mkamilifu wa hai, unapaswa kufunuliwa katika kazi yako. *Kuwa na ushirika mara kwa mara kila siku na Mungu wako, na kuisikia sauti inayokwambia, “Acheni, mjue ya kuwa Mimi ni Mungu” (Zaburi 46:10). Kadiri majukumu yenu yanavyoongezeka kwa kusonga mbele kwa ujumbe, majaribu pia yataongezeka. Kadiri ukubwa wa kazi unavyoisonga mioyo, nyenyekezeni mioyo yenu kwa Mungu. *Fanya kwa uaminifu sehemu yako katika kazi, na simama kwa uaminifu katika uwajibikaji wako binafsi mbele za Mungu. *Mungu habagui watu. Yeye atendaye haki ni mwenye haki.* Kudai kuwa muumini tu ni bure, na maarifa ni ya thamani tu ikiwa yanatumiwa kwa haki.
“Msinung’unike; msilalamike; msitamani; msigombane,” Mwalimu wetu aliendelea, *“Mnapopitia mateso, mtazameni Tabibu mkuu. mnatakiwa mfurahi, na kujinyenyekesha mbele za Bwana. Kwa kudumisha roho ya ubinafsi, watu wanaishi kwa shida na kutokuweza kuona mbali; na kisha wanashindwa kusoma toka chanzo kwenda matokeo. *Neno la Bwana yapasa liwe kiongozi wako katika mambo yote. *"Lakini BWANA yumo ndani ya hekalu lake takatifu; dunia yote na inyamaze kimya mbele zake" (Habakuki 2:20)*
*Bwana Anawaita sasa watu waliochaguliwa kwa ajili ya kazi yake kusimama kama mtu mmoja kwa ajili ya kuiendeleza kazi ya Kristo.*
*TAFAKARI NJEMA MUNGU AKUBARIKI MPENDWA*
Post a Comment