amka na Na Bwana leo 11

KESHA LA ASUBUHI

ALHAMISI, MACHI, 11, 2021
SOMO: MKRISTO MCHANGAMFU 

Kwa pendo la undugu, mpendane ninyi kwa ninyi; kwa heshima mkiwatanguliza wenzenu. 

Warumi 12:10. 



Hatuwezi kujiweka wenyewe kama vigezo ambavyo sharti wengine wavifuatishe. Tutadhihirisha upole wa moyo na shauku ya nafsi yote katika kukuza furaha ya wale wote tunaounganika nao. Tunao wajibu wa kufanya katika kuiondoa nafsi katika mipango yetu na kuhisi jukumu binafsi la kufanya kama vile ambavyo Kristo angefanya katika hali za kufanana na zile zinazotuzunguka. Kisha tutavutia fikra za wengine kwa namna ambayo Mungu atatukuzwa. 



Kama wafuasi wa Kristo tunapaswa kutafuta kufanya mguso unaovutia katika mioyo ya wale wote tulio na muunganiko nao, wa dini tunayoikiri, na kuamsha mawazo maadilifu. Baadhi wataathiriwa kwa mvuto wetu kwa wakati huu na kwa umilele.... 



Ikiwa tunaweza kufundisha wengine, sisi wenyewe inatupasa kila siku tujifunze masomo toka kwa Kristo. Kuna baadhi ambao hawatambui utakatifu wa kazi ya Mungu. Wale wenye uwezo wa chini kabisa, wasiofikiriwa na hata wale vijana wavivu hasa, wanahitaji kuzingatiwa katika maombi yetu. Tunahitaji hekima ya kipekee kujua namna ya kuwasaidia wale wasiojali na kuwafikiria wengine. Daudi alisema, "Na unyenyekevu wako umenikuza" (2 Samweli 22:36; Zaburi 18:35). 



Katika kazi ya kujitia wenyewe katika kuwasaidia wengine, tunaweza kupata ushindi wa thamani kubwa sana. Tunapaswa kujitoa wenyewe tukiwa na bidii isiyochosha, kwa uaminifu wa dhati, kwa kujikana nafsi na subira katika kazi ya kuwatia shime wale wanaohitaji kupiga hatua. Maneno ya upole yanayotia shime yatafanya maajabu. Kuna wengi ambao, ikiwa juhudi za kudumu, kwa uchangamfu, zitafanywa kwa niaba yao, pasipo kutafuta makosa au makaripio ya kudumu, wataonesha wenyewe kuwa wanaweza kupiga hatua .... 



Tunapaswa kushirikiana na Bwana Yesu katika kuwafanya upya wasio na uwezo na wanaopotoka katika akili na usafi mtakatifu. Tunaitwa na Mungu kudhihirisha mvuto usiochosha, wenye kuvumilia katika wokovu wa wale wanaohitaji uongozi wa kiungu.... Mungu hatawanyima hekima wale wanaoihitaji. Yeye humpatia mtu neema, ili naye ampatie mwingine aliye mhitaji.

No comments