IJUE MAKALA YA SADIO MANE, AMBAE NI MCHEZAJI WA LIVERPOOL NA SENEGAL (STRKER)


PART 1.

°MAKALA YA SADIO MANE (kutoka ktk wimbi la umaskini mpaka kuwa Tajiri).

Sadio Mane alizaliwa tarehe 10 mwezi wa 4 mwaka 1992 huko Sedhiou nchini Senegal.

Mane alikulia katika kijiji kidogo cha Bambali, kinapatikana kusini mwa Senegal, kilichokuwa na wakazi elfu 24,213 tu... Wakati huo Mane alikuwa akiishi na mjomba wake kwasababu wazazi wa Sadio Mane walikuwa na watoto wengi, na hawakuwa wakijiweza ki-fedha, japo mjomba nae hakuwa akijiweza ki-fedha lakini ilikuwa ni bora akae kwa mjomba wake ili kupunguza tu idadi ya watoto kule kwa wazazi wa Sadio Mane.

Kutokana na umaskini wa wazazi wake Sadio Mane walishindwa kabisa kumpeleka Sadio Mane Shule. 

Ndipo Sadio Mane akawa anaenda kucheza mpira alikuwa akiamka asubuhi kwenda mitaani kucheza mpira na jioni alikuwa akienda mitaani kucheza mpira yaani kwa siku alikuwa akienda mara mbili kucheza mpira.

Mwaka 2002, wakati huo ndo ulimshawishi sanaa Sadio Mane kuwa mchezaji maana kulikuwa na kombe la dunia, na nchi yake ya Senegal iliweza kufika robo fainali, na mechi yao ya kwanza Senegal walimfunga bingwa mtetezi ufaransa ktk mechi ya ufunguzi hio ilikuwa ni historia kubwa sanaa kwa Senegal pia kwa Sadio Mane maana ni siku ambayo ataikumbuka mpaka kesho.

Baada la kombe la dunia kumalizika mwaka huo 2002 Senegal alifika mpaka Robo fainali. 

vijana wengi wa Senegal walizidi kuvutiwa zaidi na mchezo wa mpira wa miguu baada ya Senegal kuonesha kiwango kikubwa ktk michuano ile. 

Pia kijiji cha kina Sadio Mane waliweza kuanzisha mashindano yao, kipindi wanacheza mpira wanakijiji wengi walivutiwa na uchezaji wa Sadio Mane lakini wazazi wa Sadio Mane hawakuwa wakiunga mkono hata kidogo jambo hilo... Maana wazazi wake walimtaka Sadio Mane azingatie Dini na si vinginevyo na wazazi wa Sadio Mane walikuwa ni watu wa dini sanaaa, walikuwa ni waumini wa dini ya KIISLAMU. 

Lakini Sadio Mane baada ya kupata msukumo kutoka kwa wanakijiji kuwa yeye ni mchezaji mzuri sanaa ndipo Mane akamwambia mjomba wake, kuwa mjomba nisaidie niondoke hapa kijijini niende mjini ili nikajifunze zaidii maana natamani kuwa mchezaji mkubwa hapo baadae. 

Baada ya Mjomba kuyatafakari maneno ya Mane ikabidi mjomba akaongee na dada ake pamoja na shemeji yake juu ya watamsaidiaje Mane, ndipo wazazi wa Sadio Mane ikabidi wauze mazao yao yote ili wapate pesa, pia wanakijiji waliguswa na lile jambo nao wakatoa msaada ndipo Mane akaweza kutoka kijijini kwao kwenda mpaka jiji la Dakar, wakati huo wazazi wake walijua kuwa Mane anaenda kufikia kwa rafiki yake na mjomba wake Mane lakini Ki-uhalisia Mane alikuwa anaenda huko, huku akiwa hamjui mtu yeyote yule ktk jiji hilo na ishu hio alikuwa akijua Mane na mjomba wake pekee. 

Baada ya kuchangiwa pesa na wazazi wake pamoja na wanakijiji ndipo Sadio Mane akaanza safari ya kwenda ktk jiji kubwa la Senegal bila ya kujua ataenda kufikia kwa nani....alivyofika ktk Jiji hilo moja kwa moja akaenda katika nyumba hakuwa anaijua ila alivyofika pale aliwapa pesa kidogo tu kisha akawaelezea nia yake iliyompeleka ktk jiji hilo la Dakar, familia ile ikaelewa kile alichokisema mane ndipo wakamruhusu aingie ndani na kumpa chumba cha kulala na waliahidi kuwa watamsaidia. 

Akauliza wamtajie ni klabu gani kubwa ambayo ni maarufu jijini pale ili kesho yake aende kuitembelea, ndipo wakamuelekeza. 

Kesho yake asubuhi, Sadio Mane alienda mpaka katika hio klabu, alivyofika pale alikuta vijana wengi sanaa wakifanyiwa majaribio wakati huo Mane akiwa amesimama akiwaangalia, Mara kuna mtu mzima pale alimuona Sadio Mane akamuuliza na wewe umekuja kufanya mazoezi hapa!?? Sadio Mane akamjibu ndio, yule mzee akamjibu kwa hasira unakuja kufanya majaribio na hivyo viatu!?? Sasa utawezaje kucheza na hivyo viatu, na hizo nguo ulizovaa haziendani kabisa na sare za mpira wa miguu. 

Sadio Mane akamjibu.........!!!! ITAENDELEA

#FOOTBALL_LEGENDARY

No comments