IJUE MAKALA YA SADIO MANE, ambaye ni mchezaji wa liverpool na pia wa Senegal (striker)
(Sehemu ya Pili ktk muendelezo wa historia ya Sadio Mane)
Sadio Mane akamjibu, kila unachoniona nacho hapaa kwa upande wangu ndo nilivyo weza kuvimiliki, ila nilikuwa naomba tu nafasi ya kucheza, ili nioneshe nilicho nacho uwanjani.
Yule mzee akamruhusu Mane acheze, na kwa jinsi alivyokuwa anacheza yule mzee alitokea kuvutiwa sanaa na Sadio Mane, baada ya majaribio kumalizika yule mzee akamfata Mane na kumwambia nina kuchukua ukacheze ktk timu yangu.
Baada ya misimu miwili kucheza ktk hio Academy alifanikiwa kucheza jumla ya mechi 90 huku akifunga mabao 131.
Sasa baada ya kupita misimu hio miwili, katika Academy yao ambayo ni Generation Foot, walikuja watu kutoka taifa la ufaransa ili kuja kutafuta wachezaji ambao wenye vipaji vikubwa vya mpira wa miguu lakini wanaoishi ktk umaskini.
Na walivyofika hao ma-scout ktk Academy ya Mane waliweza kuona kipaji cha Sadio Mane na wakamchukua wakampeleka mpaka ufaransa ktk klabu ya Metz wakati huo akiwa na miaka 15 tu.
Na katika klabu hio ya Metz walipita watu maarufu kama Song, Louis Saha, Adebayor, Papiss Cisse, na Robert Pires.
Lakini mpaka Sadio Mane anaenda zake Ufaransa, hakumwambia mzazi wake yeyote kama anaondoka, alipanga kuwafanyia Suprise wazazi wake,
Mpaka kufikia mwaka 2011, mama yake alikuwa anajua bado Sadio Mane anacheza ktk Academy ya Generation Foot, maana Sadio alimwambia mjomba wake tu.
Mwaka huo ndo alipanga kumwambia mama yake kuwa yupo ufaransa... Na maongezi yao yalikuwa kama hivi.
Sadio Mane 🗣️ Haloo!! Mamaa mimi ni mwanao Sadio Mane, nipo Ufaransa
Mama 🗣️ Mane mwanangu, unasema ufaransa ipi!?? au unaishi Senegal??
Sadio Mane 🗣️ Hapana mama, mimi nipo Ulaya huku nchini Ufaransa.
Baada ya hapo mama ake Sadio Mane ni kama aliyekuwa amepatwa na mshangao mkubwa juu ya mwanae kuwa nchini ufaransa, lakini mama huyo alikuwa bado haamini alikuwa akimpgia sana simu mwanae kuuliza kama ni kweli kwa kile alichokisema... Mane alikuwa akimwambia ni kweli yupo ufaransa lakini mama huyo alikuwa bado aamini, ndipo siku Sadio Mane akamwambia mama yake aende kumuangalia ktk Runinga, Hatimae mama yake alifanya kama alivyo ambiwa na mwanae ndo aliweza kumuona kwa mara ya kwanza ktk Runinga mwanae akicheza mpira barani Ulaya...
Msimu wake wa kwanza kucheza Metz, Sadio Mane alipata tabu sana kuzoea hali ya hewa ya kule maana ilikuwa ni tofauti kabisa na hali ya hewa ya Senegal, pia aliweza kupata majeraha ya Pelvic ambayo yalimuweka nje kidogo lakini licha ya yote hayo Sadio Mane hakuvunjika moyo hata kidogo maana ndoto yake kubwa ni kuja kuwa mchezaji mkubwa hapo baadae na kufikia hilo ilimradhimu kufanya mazoezi kwa bidii kila akipata nafasi hio.
Mwaka 2012, katika Michuano ya Olympic akiwa na timu yake ya Senegal alionesha performance kubwa sanaa ambayo ndo ilimfanya mpaka asajiriwe na klabu ya Red Bull Salzburg.
Baada ya kusajiriwa na Red Bull Salzburg alidumu hapo kwa misimu miwili alicheza jumla ya MECHI 80 huku akifunga MABAO 42... Kisha akaondoka zake mpaka Ligi Kuu ya EPL ambapo ndoto yake ni kwenda kucheza ktk ligi hio, na alisajiriwa na timu ya Southampton tena kwa bei ya record ya klabu ilikuwa ni £11.8 Million alicheza hapo kwa misimu miwili michezo 67 akifunga mabao 21.
Baada ya misimu miwili kupita akiwa Soton ndo Liverpool wakaamini uwezo wa Sadio Mane na kumsajiri kwa dau la £34 million wakati huo ukiwa ni mwaka 2016... Na mtu wa kwanza kumwambia kuwa anaenda timu ya Liverpool alikuwa ni mama yake.
Jurgen Klopp ndie aliefanya msisitizo mkubwa kwa Liverpool ili wamsajiri Mane maana alikuwa akimuhusudu sanaa, pia Klopp aliwahi kumwambia Mane kuwa nakuhitaji uje Liverpool.
Ndomana baada ya Liverpool kupeleka offer kule Southampton, Sadio alikataa vilabu vingine ili aende Liverpool timu ambayo inayohitaji huduma yake na kocha ambae aliona kipaji chake na kuvutiwa nacho...tangu wakati huo 2016 mpaka hivi sasa 2021 Sadio Mane anaendelea kukipiga na Liverpool.
Sadio Mane amekuwa mchezaji wa kwanza ktk historia ya EPL kufunga Hattrick ya mapema zaidi alitumia sekunde 176 tu akiwafunga Aston Villa.
Post a Comment