AMKA NA BWANA LEO 29
KESHA LA ASUBUHI
JUMATATU, MACHI, 29, 2021
SOMO: KUTOA KILE ULICHONACHO
Nafsi ya mtu mkarimu itawandishwa; anyweshaye atanyweshwa mwenyewe.
Mithali 11:25.
Uhuru ni moja ya mielekeo ya Roho Mtakatifu, na wakati wanaodai kuwa watu wa Mungu wanapomnyima mali yake mwenyewe katika zaka na sadaka, watakutana na hasara ya kiroho. Bwana hazawadii uhuru ulio nyimivu. Anawaita watu wamheshimu kwa mali zao, na kwa malimbuko ya mazao yao yote.
Haiwezekani kuweka kanuni kwa kila jambo; kwa kuwa katika mifano mingi uelekeo kama huo unaweza kumhuzunisha mtoaji. Mazingira ambayo wengine huwekwa, na ambayo Mungu mwenyewe hupanga, yanapaswa kuzingatiwa. Mungu anatarajia mtu kutoa katika kile alicho nacho na si katika asicho nacho. Kwa wengine moja ya kumi ya mapato isingewakilisha kwa kustahili uwiano wanaopaswa kumtolea Bwana, wakati kwa wengine ni urudishaji wa haki.
Ni wangapi wanaopoteza mibaraka mingi na kudumazwa kiroho kwa sababu wanamnyima Mungu yaliyo yake. Adui wa Mungu na mwanadamu yupo kazini kwa kudumu kuchepua hazina ya Mungu na kumpendeza na kumheshimu na kumtukuza wakala wa kibinadamu. Mahitaji ya familia yangu hutaka hili na lile, watu husema, huongezwa katika nyumba vitu vyenye kufaa katika samani, katika mavazi, mapochopocho kwa ajili ya meza. Wanashindwa wekea ukomo tamaa zao, wakati ambao kwa kufanya hivyo wangeleta baraka kwao wenyewe na kwa familia zao.
Bwana ametufanya watoaji sadaka wake, wenzi wake katika kazi kubwa ya kuuendeleza ufalme wake. Tunaweza kufuata nyayo za wakili asiye mwaminifu, na kwa kufanya hivyo tukapoteza fursa za thamani zilizowahi kutolewa kwa wanadamu. Kwa miaka maelfu Mungu ametenda kazi kupitia kwa mawakala wa kibinadamu, lakini kwa matakwa yake anaweza kuwaondosha wabinafsi, wenye kupenda fedha, watamanifu. Anaweza kuiendeleza kazi yake hata kama hatutashiriki kwa sehemu yoyote. Bali ni nani miongoni mwetu angefurahishwa kwa Bwana kufanya hivyo? ...
Bwana husoma kila wazo la moyo, kila msukumo wa fikra. Ikiwa hatuna roho ya kutoa kwa hiari, tunamdhihaki. Tunapoonesha kwa ulimwengu, kwa malaika, na kwa wanadamu kwamba mafanikio ya kazi ya Mungu ni kipaumbele chetu cha kwanza, Mungu atatubariki.
Post a Comment