FACTS 10 NA NUSU ZA KOCHA THOMAS TUCHEL
1️⃣-KOCHA WA 15,CHELSEA YA ROMAN.
Tuchel mzaliwa wa Agosti 29, 1973. Ni kocha wa 15 kwa Chelsea tangu bilionea wa Kirusi, Roman Abromovich ainunue klabu hiyo mwaka 2003. Alichukua nafasi ya legend wa klabu hiyo, Frank Lampard ambaye aliondoshwa kwa mfululizo mbaya wa matokeo. Tuchel ambaye ni kocha mwenye rekodi nzuri ya ushindi akiwa Dortmund na PSG pamoja na Unbeaten run akiwa Chelsea mpaka sasa alirithi kipaji cha ukocha kutoka kwa baba yake mzee Rudolf Tuchel ambaye alishawahi kumfundisha mpira kipindi cha utotoni. Anapendelea kutumia 4-3-3, 3-4-3 katika muundo wa 3-5-2 na mara chache 4-2-3-1, ni kocha anayebadilika badilika kulingana na mchezo unataka nini.
2️⃣- TUCHEL ALIWAHI KUWA MWANAMITINDO.
Tuchel ni mtu wa kujichanganya katika mambo mengi ili maisha yaende, huwezi amini mwaka 2017 alienda New York kushiriki katika tukio la wanamitindo, akishiriki upigaji picha katika jarida la wanaume wa kijerumani 'Die Zeit'.
3️⃣-ALIWAHI KUFANYA KAZI BAR, “BARMAN”.
Tuchel alikuwa ni mtu wa kutafuta mishe nyingi ili aweze kupata fedha za kujikimu, baada kushindwa kufanikiwa akiwa kama mchezaji wa mpira. Akawa anafanya kazi ya kuchanganya Cocktail hapo bar wanywaji mnaelewa hapa.
4️⃣- JINA LA UTANI “THE PROFESSOR”.
Mtaalamu huyu wa soka kutoka Ujerumani, amekuwa akiitwa "The Professor" muda mrefu katika maisha yake ya ukocha. Tuchel licha ya kujishughulisha na mambo mengine nje ya soka lakini bado aliamini bado anakitu cha kuufanyia mpira. Alimtafuta bosi wa Stuttgart wa kipindi hicho bw. Ralf Rangnick ambaye hivi karibuni alikuwa mkuu wa kitengo cha michezo pale Red Bull Football Association na ameifundisha RB Leipzig mpaka 2019, kwa ajili ya majaribio ya ukocha kwenye kikosi cha reserve ya timu hiyo. Mtaalamu Rangnick alipoona Tuchel ana akili sana ya mpira akampa nafasi, aliwafunika makocha wote katika academy hadi akapewa kikosi cha U14 mwaka 2000. Hapo ndio jina la Professor lilipoanzia.
5️⃣-ANA DEGREE YA USIMAMIZI WA BIASHARA “Business Administration”.
Akiwa na miaka 19 aliachwa na klabu ya Augsburg, akaenda ligi daraja la pili katika timu iliyoitwa Stuttgarter kickers akacheza mechi nane tu klabuni hapo. Maisha yake ya uchezaji yakaendelea kuwa ya mashaka mashaka akaenda katika klabu ya ligi daraja la tatu, SSV Ulm ambako alilazimika kutundika daruga akiwa na miaka 24 tu baada ya kupata majeraha ya goti. Hakukubali kuishi katika ndoto zilizofeli akaingia kwenye chuo kimoja ambapo alienda kusomea usimamizi wa Biashara.
6️⃣-NDOTO YA URUBANI WA HELICOPTER.
Akiwa mdogo kabisa, wakati anasoma huku akicheza mpira chini ya uangalizi wa baba yake ambae alikuwa kocha wao. Tuchel alikuwa na ndoto za kuwa pilot kama mbadala wa mambo ya mpira, na hiyo ndo inatajwa sababu ya Tuchel kutokuacha kusoma kwa wakati huo licha ya kuwa na ratiba ngumu kwenye academy ya mpira. Alijibana kadri awezavyo apate muda wa shule na muda wa kucheza soka.
7️⃣-SAKATA LA UZITO MDOGO.
Unaambiwa mwaka 1988 akiwa na miaka 15, mwaka ambao alifanikiwa kufuzu majaribio ya kucheza soka katika academy ya FC Augsburg. Alipopimwa uzito alikuwa na kilogramu 28 akiwa na urefu wa mita 1.4. Hivi hata muda huu kwa ule wembamba wake tukimkadilia atakuwa na kilo ngapi?.
8️⃣-TUCHEL ANAPENDA SAIKOLOJIA.
Tuchel, ni moja ya makocha wanaoamini kuwa saikolojia ndiyo inatanabaisha kiwango cha mchezaji uwanjani. Akiwa Mainz aliwahi kuwapima wachezaji wake akili “Mental test” ambapo alikuja na tathmini yenye kurasa 30. “Hatutakiwi kuishia kutofautisha mazoezi kwa mchezaji mmoja mmoja, tunatakiwa pia kutofautisha hata namna ya kuongea na wachezaji wetu” Tuchel alimwambia Christopher Berman ambaye ni mwandishi wa mpira "Football Writer" alipokuwa akiandaa kitabu chake kiitwacho (Football Hackers: The science and Art of Data Revolution).
9️⃣-KWANINI ALISTAAFU MAPEMA SOKA?Tuchel alikuwa beki, katika safari yake ya mpira kama nilivyotaja hapo juu alipokuwa SSV Ulm Tuchel alipata majeraha makubwa ya goti. Ambayo pamoja na jitihada zote alishindwa kupona vizuri kiasi cha kuamua kustaafu soka akiwa na miaka 24 tu. Hii ikiwa na maana alicheza soka la kulipwa kwa kipindi cha miaka mitano tu.
🔟-GEGENPRESSING.
Tuchel nae ni moja ya makocha wanaotumia falsafa maarufu ya kijerumani "Gegenpressing" falsafa ambayo Ralf Rangnick ndiye anayetajwa kuwa kocha wa mwanzoni kabisa kutumia miaka hiyo ya zamani. Na ikaja kuwa maarufu chini ya mtangulizi wake pale Mainz na Dortmund, Jurgen Klopp.
Mwaka 2009, akiwa hafahamiki sana alichaguliwa kuichukua nafasi ya Klopp pale Mainz na miaka 6 baadae akaja kuchukua nafasi yake pale Dortmund pindi Jurgen alipoamua kutimkia Liverpool.
Kwa uchache hii gegenpressing ni namna ambapo timu inausaka mpira punde inapopoteza na kuanza kutengeneza mashambulizi. Timu inakuwa inakabia eneo la juu wanapokuwa hawana mpira huku wakifuata mpira katika eneo la chini kabisa la timu pinzani kwa kasi hadi waupate mpira.
🔟½ - Professor Tuchel licha ya kuwa mtu anayezingatia sana saikolojia ya wachezaji lakini pia ni mtunzaji mzuri wa takwimu na anazingatia sana utimamu wa mwili kwa wachezaji anaowafundisha. PSG ya Tuchel ilifunga mabao 337 katika mechi 127. Dortmund ya Tuchel ilifunga mabao 251 katika mechi 107. Chelsea ya Tuchel imefunga mabao mangapi hadi sasa?
Post a Comment