UTACHANGANYIKIWA KUWA MAKINI

_*"Nimeonyeshwa kwamba wengi wa wale wanaojidai kuwa na maarifa ya ukweli wa leo HAWAJUI NINI WANACHOKIAMINI. HAWAELEWI VITHIBITISHO VYA IMANI YAO. Hawana UTHAMINI WA KAZI YA WAKATI WA SASA. Wakati wa kujaribiwa utakapofika, KUNA WATU SASA WANAHUBIRI KWA WENGINE WATAKAOJIKUTA, KATIKA KUJITATHMINI MSIMAMO WANAOUSHIKIRIA, kwamba KUNA VITU VINGI HAWAWEZI KUTOA SABABU ZINAZOJITOSHELEZA. Hadi pale wanapojaribiwa ndipo wanakuja kujua ujinga wao mkuu." (Maranatha. uk.45.2).*_

*"Na kuna wengi kanisani ambao huchukulia ni haki yao kwamba  WANAJUA WANACHOKIAMINI; LAKINI, HADI PALE PAMBANO LINAPOINUKA, NDIPO WANAJUA UDHAIFU WAO WENYEWE. Wanapotenganishwa na wale wenye imani sawa na kulazimika KUSIMAMA PEKE YAO NA MMOJA MMOJA kuelezea imani yao, WATASHANGAZWA KUONA JINSI GANI WANACHANGANYIKIWA JUU YA UFAHAMU WA KILE WALICHOKIPOKEA KAMA KWELI." ( Maranatha. uk.45.2).*_

*"Mungu atawaamsha watu wake; WAKATI NJIA ZINGINE ZINASHINDWA, MADANGANYO YATAKUJA MIONGONI MWAO, Ambayo yatawapepeta, yakitenganisha kati ya magugu na ngano. Bwana anaita juu ya wote waaminio neno KUAMKA TOKA USINGIZINI. NURU YA THAMANI IMEKUJA, MAALUMU KWA WAKATI HUU.....Waumini hawapaswi kulala katika mapendekezo na hoja dhaifu za kile kinachounda  kweli. IMANI YAO INAPASWA KUSIMIKWA IMARA JUU YA NENO LA MUNGU ili kwamba wakati wa kujaribiwa ufikapo na WATAKAPOLETWA MBELE YA MABARAZA KUJIBU kwa ajili ya imani yao waweze kutoa sababu kwa ajili ya tumaini lao kwamba lililo ndani yao kwa upole na kicho. (Maranatha. uk. 45.3).*

No comments