amka na Bwana leo 24
KESHA LA ASUBUHI
JUMATANO, MACHI, 24, 2021
SOMO: MKRISTO MWENYE MSIMAMO
Mungu ni nuru, wala giza lolote hamna ndani yake.... Bali tukienda nuruni, kama yeye alivyo katika nuru, twashirikiana sisi kwa sisi, na damu yake Yesu, Mwana wake, yatusafisha dhambi yote.
1 Yohana 5,7,
Ni upendeleo wa Mkristo kuunganika na chanzo cha nuru, na kupitia muunganiko huu ulio hai anakuwa nuru ya ulimwengu. Mfuasi wa kweli wa Kristo atatembea nuruni kama yeye alivyo nuruni na kwa hiyo hawatatembea katika njia isiyo ya uhakika, na kujikwaa kwa sababu wanatembea gizani. Mwalimu Mkuu anatia kwenye fikra za wasikilizaji wake baraka wanayoweza kuwa kwa ulimwengu, akiwakilishwa kama jua linalochomoza toka mashariki, ikifukuza ukungu na vivuli vya giza.
Mapambazuko huipisha mchana. Jua, liking’aa kwa uzuri, likitia rangi, na kisha kuzitukuza mbingu kwa miali yake ya nuru ni mfano wa maisha ya Ukristo. Kama vile mwanga wa jua ni nuru na uhai na baraka kwa wale wote wanaoishi, vivyo hivyo Wakristo, kwa matendo yao mema, kwa uchangamfu wao na ujasiri, wawe nuru ya ulimwengu. Kama vile mwanga wa jua ufukuzavyo vivuli vya usiku na kumwaga utukufu wake katika mabonde na milima, vivyo hivyo Wakristo huakisi Jua la Haki inayoangaza kwao.
Mbele ya maisha yenye msimamo ya wafuasi wa kweli wa Kristo, ujinga, uchawi, na giza vitapita, kama vile jua lifukuzavyo utusitusi wa usiku. Kwa jinsi hiyo hiyo wanafunzi wa Yesu wataenda katika maeneo yenye giza duniani, wakieneza nuru ya kweli hadi njia ya wale walio gizani itakapomulikwa kwa nuru ya kweli.
Kuna tofauti kubwa kati ya hao na maisha ya yule anayekiri kuwa mtoto wa Mungu ambaye ni chumvi isiyo na ladha. Hana muunganiko muhimu na Mungu na, kama chumvi isiyofaa —ambayo Kristo huelezea kama isiyofaa kitu tokea hapo bali kutupwa na kukanyagwa na watu —anakosa sifa. Hayo ndiyo maisha ya anayekiri kuwa mfuasi wa Kristo ikiwa hana muunganiko ulio hai na Yesu Kristo. Hawa wanaodai kuwa na imani bila kuwa na jua ni vivuli vya giza....
Kila udhihirisho wa mashaka huimarisha kutokuamini. Kila wazo na neno la matumaini, ujasiri, nuru, na upendo huimarisha imani na kuimarisha moyo kustahimili giza la kimaadili lililopo duniani. Wale wanaozungumza imani watakuwa na imani, na wale wanaozungumza kukata tamaa watakatishwa tamaa. Kwa kutazama tunabadilishwa.
Post a Comment