mafunzo ya watu wazima leo 24

LESONI, MACHI 24

SOMO: JUMUIA YA WAUMINI (ISA. 66:21) 



Waisraeli walikuwa “ ufalme wa makuhani, na taifa takatifu.” (Kutoka 19:6), wakiwa na makuhani maalumu waliotengwa rasmi kuwawakilisha kama viongozi wa ibada. Lakini siku za usoni, baadhi ya watu wa Mataifa watafanyika viongozi wa ibada (Isa. 66:21). 



Badiliko hili litaathirije jumuia mpya ya waumini? Soma Mathayo 28:19, Matendo 26:20, Gal. 3:28, Kol. 3:11, 1 Tim. 3:16.



Katika “mpango mpya” wa Mungu, watu wa Mataifa siyo tu kwamba watajiunga na watu wa Mungu, ila pia watakuwa washirika sawa na Wayahudi katika jumuia ya waumini inayounda “ukuhani wa kifalme.” Hivyo tofauti kati ya Wayahudi na Mataifa itakuwa aipo. 



Ni lini unabii huu wa Isaya utatimilika?

Paulo, mtume kwa watu wa Mataifa, alitamka: “Hapana Myahudi wala Myunani. Hapana mtumwa wala huru. Hapana mtu mume wala mtu mke. Maana ninyi nyote mmekuwa mmoja katika Kristo Yesu. Na kama ninyi ni wa Kristo, basi, mmekuwa uzao wa Ibrahimu, na warithi sawasawa na ahadi.” (Gal. 3:28, 29). 



Kuwa warithi wa imani na hivyo kujumuika katika “ukuhani wa kifalme” lilikuwa siyo suala la kujiona bora bali lilikuwa agizo la injili kuungana na Wayahudi kutangaza: “fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu” (1 Pet. 2:9; linganisha na Isa. 66:19). 



Kuwainua Mataifa haikuwafanya Wayahudi walalamike kwamba Mungu hakutenda haki kuwapatia thawabu kuu hiyo. Wala Mataifa hawakupaswa kuwabeza ndugu na dada zao Wayahudi, kama vile watendakazi walioajiriwa asubuhi hawakupaswa kuwalaumu wenzao walioajiriwa jioni. (soma Mathayo 20:1—16). Wayahudi ndio wao walikabidhiwa kwanza “mausia ya Mungu” (Rum. 3:2) kama mfereji wa ufunuo wa Mungu. 


Paulo aliwaandikia Mataifa: “Lakini iwapo matawi mengine yamekatwa, na wewe mzeituni mwitu ulipandikizwa kati yao, ukawa mshirika wa shina la mzeituni na unono wake, usijisifu juu ya matawi yale; au ikiwa wajisifu, si wewe ulichukuaye shina, bali ni shina likuchukualo wewe” (Rum. 11:17, 18)

No comments