amka na Bwana leo 25
KESHA LA ASUBUHI
ALHAMISI, MACHI, 25, 2021
SOMO: KUTENGENEZA USAWA WA JARIBU LAKO.
Jaribuni mambo yote; lishikeni lililo jema.
1 Wathesalonike 5:21.
Ndugu, ni lazima tuzame chini zaidi kwenye shimo la mgodi wa kweli. Unaweza kuuliza masuala yanayokusumbua binafsi na ninyi kwa nini, ikiwa tu utafanya kwa nia sahihi; lakini mara nyingi nafsi ni kubwa, na mara tu uchunguzi unapoanza, nia isiyo ya Kikristo hudhihirishwa. Hili ndilo Shetani hulifurahia, lakini tunapaswa kuja kwa moyo wa unyenyekevu ili tujue kwa ajili yetu wenyewe kilicho kweli.
Wakati unakuja ambapo tutatengwa na kutawanywa, na kila mmoja wetu atapaswa kusimama bila kuwa na fursa ya ushirika na wale wenye imani ya thamani sawa; na unawezaje kusimama ikiwa Mungu hayuko upande wako, na kujua kuwa anakutangulia njia na kukuongoza? Kila tunapokuja kuichunguza kweli ya Biblia, Bwana wa makusanyiko yu pamoja nasi. Bwana haachi meli hii kuongozwa na marubani wasio na ufahamu. Tunaweza kupata maagizo yetu kutoka kwa Nahodha wa wokovu wetu....
Ikiwa ndugu anafundisha makosa, wale wanaowajibika katika nafasi zao wanapaswa kulijua; na ikiwa anafundisha kweli, wanapaswa kusimama pamoja naye. Wote ni lazima tujue kile kinachofundishwa miongoni mwetu, kwa kuwa ikiwa ni kweli, tunahitaji kuijua. Mwalimu wa Shule ya Sabato anapaswa kuijua, na kila mwanafunzi wa Shule ya Sabato anapaswa kuielewa.
Wote tuko chini ya wajibu kwa Mungu kujua kile anachotutuma. Ametoa mielekeo ambayo kwayo twaweza kupima kila fundisho —“Na waende kwa sheria na ushuhuda; ikiwa hawasemi sawasawa na neno hili, bila shaka kwa hao hapana asubuhi” (Isaya 8:20). Lakini ikiwa ni kulingana na kipimo hiki, usijazwe sana chuki isiyo na sababu kwamba huwezi kukubali wazo linapothibitishwa kwako, kwa sababu tu haipatani na mawazo yako.
Usisikilize kila pingamizi, hata kama dogo kiasi gani, na kulifanya kubwa sana, na kulihifadhi kwa matumizi ya wakati ujao. Hakuna aliyesema kwamba tutapata ukamilifu kulingana na kila uchunguzi wa mwanadamu, bali hili nalijua, kwamba makanisa yetu yana shauku kubwa ya uhitaji wa mafundisho juu ya somo la haki kwa imani katika Kristo, na kwa ajili ya kweli zinazofanana.
Haijalishi ni kupitia kwa nani nuru imetumwa, ni lazima tufungue mioyo yetu kuipokea katika upole wa Kristo.
Post a Comment