amka na Bwana leo 14
KESHA LA ASUBUHI
JUMAPILI, MACHI, 14, 2021
SOMO: BARAKA ZA MZALIWA WA KWANZA
Nitakufundisha na kukuonyesha njia utakayoiendea; Nitakushauri, Jicho langu likikutazama.
Zaburi 32:8.
Kuna upendeleo mwingi wa kila mshiriki mmoja wa kanisa kujua toka katika Neno mapenzi ya Mungu kuhusiana na namna yake ya utendaji kama vile ilivyo kwa mwenyekiti wa konferensi au kwa mtu mwingine yeyote katika ofisi ya dhamana. Bwana anapaswa kutafutwa na wote ambao wangetaka kuelekezwa na kuelimishwa na kutendewa kazi na Roho Mtakatifu. Mungu yuko tayari kufanya ushirika na watu wake....
Kila mtu ni lazima atafute kwa maombi ya dhati kulijua Neno la Mungu kwa ajili yake mwenyewe, na kisha kulitenda. Ni kwa kuliweka tumaini lake kwa Mungu siku kwa siku tu, na si kwa nguvu za kibinadamu, nafsi yoyote itapata uzoefu wenye manufaa kwa ajili ya kujibu ombi la Kristo, “Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma” (Yohana 17:3). Hili ndilo fundisho linalotolewa kwa kila nafsi iliyoanza mwaka mpya.
Katika matatizo yako yote ya duniani, katika taabu yako yote na wasiwasi, mngoje Bwana. Msiwatumainie wakuu wala wana/ binadamu kwa kuwa wanaweza kuwa katika nafasi za dhamana. Bwana ameunganisha moyo wako na Yeye. Ikiwa unampenda, na kupokelewa katika utumishi wake, leta mizigo yako yote, ya wazi na binafsi, kwa Bwana na umngojee. Kisha utakuwa na uzoefu binafsi, uthibitisho wa uwepo wake na utayari wake kusikia maombi yako kwa ajili ya hekima na maelekezo yatakayokupa uhakikisho na ujasiri katika utayari wa Bwana kukusaidia katika mafadhaiko yako....
Angependa uwe mwenye furaha na kumsifu kila siku kwa ajili ya upendeleo uliopatiwa katika maneno Kristo, “Njooni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha” (Mathayo 11:28).... Weka wazi tatizo lako mbele za Bwana, na wasiwasi wako wowote na majaribu, roho yako itatiwa nguvu kwa ajili ya ustahimilivu. Njia itafunguliwa mbele yako na kwa ajili yako mwenyewe kutolewa katika aibu na ugumu. Hupaswi kwenda katika mji unaofuata au miisho ya dunia kujifunza ni mwelekeo gani utakaochukua. Mtumaini Mungu kama msaidizi wako wa sasa, atakayebatilisha mambo yote kama yeye ajuaye vizuri kabisa.
Post a Comment