Mafunzo ya watu wazima leo 14

LESONI, MACHI 14

SOMO: MADHARA YA DHAMBI (ISAYA 59) 



Katika Isaya 58:3 watu walimwuliza Mungu: “Mbona tumefunga, lakini huoni? Mbona tumejitaabisha nafsi zetu, lakinj huangalii?” 



Kinyume chake, Isaya 59:1 hutoa jibu kwa swali ambalo linaelekea kuwa kama ifuatavyo: “Kwa nini tumeita mkono wa BWANA upate kutuokoa, ila hakutuokoa? Kwa nini tunamlilia, lakini hatusikilizi? Isaya anawajibu kuwa: “Tazama, mkono wa Bwana haukupunguka, hata usiweze kuokoa wala sikio lake si zito, hata lisiweze kusikia” (Isa. 59:1). Yeye anao uwezo, ila kushindwa kwake kutekeleza hayo, kunatokana na sababu nyingine maalumu kabisa. 



Soma Isaya 59:2. Ni ujumbe gani unatolewa hapa wenye kujibu swali lililoulizwa katika Isaya 59:1?



Mungu ameamua “kuwaacha” watu wake, siyo kwa vile hiyo ndiyo shauku yake, bali kwa vile: "maovu yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu" (Isa. 59:2). Hapa twaona kauli moja katika Biblia yenye kuelezea wazi madhara ya dhambi katika mahusiano ya Mungu na mwanadamu. Isaya anatumia sehemu iliyosalia ya sura ya 59 kuelezea kwa kinagaubaga jambo hili, ambalo hujitokeza kwenye historia yote ya mwanadamu. Dhambi itaathiri mahusiano yetu na Mungu na hivyo kutuletea uangamivu wa milele—siyo kwamba dhambi humfukuzia Mungu mbali nasi bali kwamba hutufukuza sisi mbali na Mungu. 



Soma Mwanzo 3:8. Je kielelezo hiki hufunuaje kanuni iliyoelezewa kwenye ibara hiyo hapo juu?



Dhambi kimsingi humaanisha kumkataa Mungu, kumgeuzia kisogo. Tendo la dhambi ni matokeo halisi ya kumgeuzia Mungu kisogo hivyo kumfanya mwenye dhambi azidi kutanga mbali na Mungu. Dhambi hututenga mbali na Mungu, siyo kwamba Mungu hawezi kumtafuta mwanadamu (kwa kweli, Biblia nzima ni jitihada za Mungu kumtafuta mwenye dhambi apate kumwokoa) ila kwa vile dhambi hutusababisha sisi kugeuzia kisogo jitihada za Mungu kututafuta. Hii ndiyo sababu ni muhimu kutokumbatia dhambi yo yote maishani mwetu. 



Ni kwa jinsi gani umepitia uzoefu kuwa dhambi inatutenga mbali na Mungu? Kwako binafsi, unafikiri ni nini suluhisho pekee kwa tatizo hilo? 

No comments