MSITOE TAARIFA KWA UMA ZISIZOKUWA NA MIONGOZO YA KIAFYA

“Nazikumbusha Taasisi zote za Umma, Taasisi za Kidini, Taasisi Binafsi, Taasisi za Kijamii na Vyombo vyote vya Habari kuepuka kutoa taarifa za Afya ambazo hazifuati miongozo ya Wizara, wakishatoa taarifa hizo zinazua taharuki na hofu kwa Jamii”-WAZIRI GWAJIMA

“Baadhi ya bidhaa za Tiba Asili zilizohakikiwa na Mkemia Mkuu kuwa ni salama ni pamoja na Covidol, Bingwa,Nimcaf,Planet, Uzima,Bupiji n.k, hizi ni baadhi tu kesho Baraza la Tiba Asili litataja nyingine, hizi ni silaha zetu tumepewa na Mungu kama Nchi nyingine walivyopewa”-GWAJIMA 

“Nalielekeza Baraza la Tiba Asili, kwa ushirikiano na Watengenezaji wa bidhaa za Tiba Asili ambazo zimehakikiwa na Mkemia wa Serikali, kesho lifafanue zaidi juu ya bidhaa hizo kuwa zinafaa kwa matumizi na zinawaponya wengi au kuwapa nafuu, lengo Watu wajue zinakopatikana”-GWAJIMA 

“Kuhusu mbinu za kujikinga na Corona, Wananchi wajielekeze kwenye Elimu inayotolewa na Wataalamu wa Afya ikiwemo kuimarisha usafi wa mazingira na wa Mtu mmojammoja, kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni, sanitizer,Lishe,kujifukiza,mazoezi, matumizi ya Tiba asili n.k”-GWAJIMA 

“Kwa sasa Wizara haina mpango wa kupokea chanjo ya Corona inayoripotiwa kuwepo na kutumika kwenye Mataifa mengine, Serikali kupitia Wizara inazo taratibu zake za kufuata inapotaka kupokea bidhaa za afya, baada ya kujiridhisha, kwa nia njema kabisa ni hadi tujiridhishe”-GWAJIMA
#BinagoUPDATES 

No comments