usaliti katika kanisa

USALITI MIONGONI MWA VIONGOZI WA KANISA.[sda]

Nyota nyingi ambazo tulikuwa tunaziheshimu na kuzipenda kwasababu ya mng'ao wao zitazimika na kuwa giza. PK 188 ( C 1914)

Watu ambao MUNGU  aliwaheshimu sana, katika harakati za kufunga historia ya dunia, watafuata mfano wa israeli ya zamani , kujitenga na kanuni KUU ambazo KRISTO amedhihirisha katika mafundisho yake, utimizaji wa miradi ya kibinadamu, kutumia maandiko ili kuhalalisha mwenendo mbaya chini ya utendaji mbovu wa Lusifa, utawashupaza watu katika kutoelewana, na ukweli wanaouhitaji ili kuwahifadhi dhidi ya matendo mabaya utavuja na kumwagika kutoka rohoni kama maji kwenye chombo kinachovuja. 13 MR 379, 381 (1904)

Wengi watadhihirisha kuwa hawako pamoja na Kristo , kwamba hawajaufia ulimwengu , ili waweze kuishi naye, na UASI WA WATU WALIOBEBA NYADHIFA ZA UONGOZI UTATOKEA MARA KWA MARA. RH SEPT 11,1888

#WACHUNGAJI WASIOJITAKASA #WATAONDOLEWA.
..................................................................

Jambo kuu lililo karibu sana kutokea [ulazimishaji wa sheria za Jumapili] litawaondoa wale ambao MUNGU hakuwateua, naye atabakiwa na wahudumu waliojitoa wakfu, wa kweli na safi, waliojiandaa kwaajili ya mvua ya masika. 3SM 385 (1886)

Wengi watasimama katika mimbari zetu wakiwa na TOCHI YA UNABII WA UONGO MIKONONI MWAO, ILIYOWASHWA KUTOKA KWENYE TOCHI YA SHETANI YA JEHANAMU.

Baadhi watajitenga nasi na hawataendelea tena kulibeba sanduku. Lakini hawa hawawezi kujenga kuta za kuuzuia  ukweli, kwa maana utasonga mbele na kwenda juu mpaka mwisho. TM 409, 411 (1898)

WACHUNGAJI na Madaktari wanaweza kujitenga na imani, kama neno lisemavyo kuwa WATAJITENGA na kama vile ujumbe ambao MUNGU amempatia mtumishi wake usemavyo kuwa Watajitenga. 7MR 192 (1906)

Nawaambieni, si WACHUNGAJI wachache wanaosimama mbele ya Watu kufafanua maandiko walio na Unajisi, . MIOYO YAO IMEJAA UFISADI, MIKONO YAO NI MICHAFU. 5T 78 [1882]

No comments