JPM; TUACHE UBAGUZI TUHIMIZE NA KUIPENDA LUGHA YETU YA KISWAHILI
Rais Dkt. Magufuli ameihimiza mahakama kitumia lugha ya Kiswahili katika shughuli zake, kwani wanapotumia lugha ya Kiingereza wanawaongezea wananchi gharama ya kutafsiri.
Kuandika hukumu kwa Kiswahili siyo dhambi, hii pia inatia dosari kwenye uhuru tulionao."- Rais Magufuli.
Sasa wakati umefika wa kuanza kuweka mikakati ya lugha ya Kiswahili kutumika katika masuala ya Kimahakama na Kisheria katika ngazi zote, Kiswahili kinatumika AU, SADC, EAC nk, sioni sababu ya kwanini Mahakama hamtaki kutumia Kiswahili - JPM
Jaji Mkuu hapa umezungumza Kiswahili kizuri kuliko changu cha Kisukuma, lakini ukienda kuhukumu unaandika Kiingereza, hicho Kiswahili kimepotelea wapi?, hii ni changamoto kubwa, lazima tubadilike na tukipende kilicho chetu - JPM
#BinagoUPDATES
Post a Comment