MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI KISUTU IMEPANGA KUTOA HUKUMU KWA MBUNGE WA VITI MAALUM HALIMA MDEE
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imepanga kutoa hukumu dhidi ya mbunge wa viti maalum, Halima Mdee ifikapo Februari 25, 2021
Ni baada ya upande wa mashtaka na ule wa utetezi kufunga ushahidi wao.
Mdee anakabiliwa na shtaka moja la kutoa lugha chafu dhidi ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli.
Uamuzi huo umetolewa leo, Februari 17, 2021 na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Thomas Simba baada ya Mdee kumaliza kujitetea.
#BinagoUPDATES
Post a Comment