mafunzo ya watu wazima leo 4
*LESONI LEO.*
Alhamisi, 04/02/2021.
Usomaji wa Biblia: Ezekieli 44.
*SOMO: USHINDI WA MWISHO WA SAYUNI (ISAYA 24 —27).*
Baada ya maonyo dhidi ya mataifa mbalimbali katika Isaya 13—23, Isaya 24—27 huelezea kushindwa hatimaye kwa maadui wa Mungu ulimwenguni kote na ukombozi wa watu Wake.
Kwa nini maelezo ya Isaya ya uharibifu wa dunia (Isaya 24) yanafanana na maelezo ya Yohana ya matukio yanayohusiana na miaka 1,000 inayofuata baada ya ujio wa pili wa Kristo (Ufunuo 20)?
Kama ilivyo katika Isaya 13—14, mambo yahusuyo Babeli halisi hutumika pia kumaanisha tawala za baadaye, na “mfalme wa Babeli” huwakilisha muungano wa watawala wa kibinadamu na akili iliyoko nyuma yao, yaani Shetani mwenyewe. Hivyo, ujumbe kuwa Babeli umeanguka (Isa. 21:9) unaweza kurudiwa baadaye (Ufu. 14:8, Ufu. 18:2), na Shetani hatimaye anaangamizwa baada ya ujio wa pili wa Kriso (Ufu. 20:10). Wakati kuangamizwa kwa Babeli halisi kulikuwa “siku ya BWANA” ya hukumu (Isa. 13:6, 9), “siku kuu ya kutisha ya BWANA” nyingine (Yoeli 2:31, Mal. 4: 5, linganisha na Sefania 1:7) iko njiani.
Hali kadhalika, katika Isaya 24 njozi ya nabii inapitia katika hali ambazo anazijua hadi wakati ambapo “mwezi utatahayari, na jua litaona haya; kwa kuwa Bwana wa majeshi atatawala katika mlima wa Sayuni, na katika Yerusalemu” (Isa. 24:23). Isaya, bila shaka, alifikiri, njozi ilihusu Yerusalemu aliyoijua, lakini kitabu cha Ufunuo huelezea kuwa itatimizwa hasa katika Yerusalemu Mpya (Ufu. 21:2). “Na mji ule hauhitaji jua wala mwezi kuuangaza, kwa maana utukufu wa Mungu huutia nuru, na taa yake ni Mwana—Kondoo” (Ufu. 21:23).
Je, ni Mungu hasa anayewaangamiza waovu?
Tazama Isaya 28:21, ambapo kazi ya Mungu ya kuangamiza ni “tendo” la ajabu. Ni jambo la ajabu Kwake, kwa sababu hataki kulifanya, lakini, hata hivyo, ni tendo. Ni kweli kuwa dhambi ina mbegu za kujiangamiza yenyewe (Yakobo 1:15). Lakini kwa kuwa Mungu ana mamlaka ya mwisho juu ya uzima na mauti, na anaamua muda, mahali, na aina ya maangamizi ya mwisho (Ufunuo 20), hakuna sababu ya msingi ya kubishana kuwa hatimaye Mungu anamaliza tatizo la laana ya dhambi kwa kuruhusu kisababishi na madhara kufuata mkondo wake wa asili.
*Tunachokiona katika Isaya 24—27 ndicho tunachokiona katika Biblia nzima, ambacho hata kama kuna mateso, maumivu, na ukiwa sasa, mwishoni Mungu na wema atashinda uovu. Ni jambo gani pekee, basi, tunaweza kulifanya ili sisi nasi tuwe na sehemu katika ushindi wa mwisho? Mithali 3:5—7, Rum. 10:9.*
🙏🙏🙏🙏
Post a Comment