MAFUTA KUPANDA BEI
Watumiaji wa mafuta ya taa, dizeli na Petroli watatakiwa kuongeza kiasi cha pesa watakapohitaji bidhaa hizo baada ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji(Ewura) kutangaza ongezeko la bei mwezi Februari lililochangiwa na kupanda bei ya mafuta hayo katika soko la dunia.
Wanunuzi wa rejareja wa mafuta ya Petroli watatakiwa kuongezeka Tsh. 53 zaidi kwa lita, kuongeza Tsh. 134 zaidi lita ya Dizeli huku watumiaji wa Mafuta ya Taa wakitakiwa kuongeza Tsh. 119 kwa lita ikilinganishwa na bei ya mwezi Januari.
Wanunuzi wa mafuta kwa jumla wataongeza Tsh. 52.90 kwa lita ya Petroli, Tsh. 133.36 kwa kila lita ya Dizeli na Tsh. 118.31 kwa kila lita ya Mafuta ya Taa.
#BinagoUPDATES
Post a Comment