mafunzo ya watu wazima leo 28

LESONI, FEBRUARI 28

SOMO: UKWELI UNAOPIMA WA ISAYA (ISA. 50:4—10) 



Ikiwa Isaya alikusudia kutoa ujumbe tu, angetoa mpangilio wa habari kuhusiana na Masihi mara moja. Lakini ili kufundisha, kushawishi na kuwawezesha wasomaji wake kukutana na mtumishi wa Bwana, hujenga ubunifu mzuri wa visa vinavyojirudia katika mtindo wa simfoni(aina ya muziki wa ala nyingi). Anafunua ujumbe wa Mungu hatua kwa hatua ili kwamba kila nyanja iweze kueleweka kwa muktadha wa sehemu iliyobaki ya masimulizi. Isaya ni msanii ambaye picha yake ni nafsi ya msikilizaji wake. 



Soma Isaya 50:4—10. Fupisha kile mafungu haya yanachosema, Unamwonaje Yesu katika mafungu haya?



Tumejifunza katika Isaya 49:7 kwamba mtumishi wa Mungu anadharauliwa, anachukiwa, na “mtumishi wa watawalao” lakini kwamba " 'Wafalme wataona watasimama, ; wakuu nao watasujudu' " Hapa katika Isaya 50, tunajifunza kwamba bonde lina kina kirefu sana kwa mwalimu mpole ambaye maneno yake humtegemeza aliyechoka (Isa. 50:4). Njia ya kuelekea katika kuthibitishwa hupitia katika kunyanyaswa kimwili (Isa. 50:4). 



Huku kunyanyaswa husikika vibaya kwa wale tutokao katika utamaduni wa kimagharibi. Lakini katika utamaduni wa Mashariki ya Karibu ya kale, heshima ilikuwa suala la kufa na kupona kwa mtu na kundi lake. Ikiwa ulimtukana na kutomtendea mtu vizuri namna hii, ulipaswa kulindwa vizuri; vinginevyo, wakipata nafasi kidogo tu, mhanga na/au ukoo wake wangeweza kulipiza kisasi. 



Mfalme Daudi alivamia na kuishinda nchi ya Amoni (2 Samweli 10:1—12) kwa sababu tu mfalme wake aliwashikilia watumishi wa Daudi, akawanyoa nusu ya ndevu zao, akawachania nguo zao katikati, hata matakoni, akawatoa waende zao” (2 Sam. 10:4). Lakini katika Isaya 50 watu wanampiga mtumishi, wanang’oa kwa uchungu ndevu zake, na kumtemea mate. Kinachofanya matendo haya kuwa ya kimataifa, tukio la kiulimwengu ni kuwa mhanga ni mjumbe wa Mfalme wa wafalme, mtukufu. 



Kwa hakika, kwa kulinganisha Isaya 9:6, 7 na Isaya 11:1—16 na mafungu mengine ya “mtumishi,” tuliona kwamba mtumishi ni Mfalme, Mkombozi mwenye nguvu! Lakini pamoja na uwezo huu na heshima, kwa sababu isiyofikirika, hajiokoi Mwenyewe! Hii inashangaza kiasi cha watu kushindwa kuamini. Kwenye msalaba wa Yesu, viongozi walimdhihaki: " 'Aliokoa wengine; na ajiokoe mwenyewe, kama ndiye Kristo wa Mungu, mteule wake!' " (Luka 23:35); " 'Na ashuke sasa msalabani, nasi tutamwamini' " (Mt. 27:42). 



Pitia Isaya 50:4—10. Andika kanuni za kiroho zilizofafanuliwa hapa zinazopaswa kutumiwa katika maisha yetu wenyewe. Jitazame katika mwanga wa orodha yako. Ni katika maeneo gani unapofanya vizuri? Ikiwa umekatishwa tamaa, basi endelea kusoma kwa juma lote. 

No comments