amka na Bwana leo 28

KESHA LA ASUBUHI

JUMAPILI, FEBRUARI, 28, 2021
SOMO: WASAIDIZI WA MCHUNGAJI 

Atalilisha kundi lake kama mchungaji, Atawakusanya wanakondoo mikononi mwake; Na kuwachukua kifuani mwake, Nao wanyonyeshao atawaongoza polepole. 

Isaya 40:11. 



Katika uumbaji unaoonekana, hekima ya kiungu inadhihirishwa katika hatua za aina mbalimbali zisizo na kikomo. Kuwa sawa si sheria inayofuatwa katika ufalme wa asili. Wala si sheria inayofuatwa katika ufalme wa neema. Kwa namna tofauti Mungu hutenda kazi kulifikia kusudi moja —kuokoa roho. Kwa mbinu tofauti tofauti Mwokozi mwenye huruma hushughulika na akili tofauti tofauti. Badiliko la moyo kwa hakika linaletwa kwa mchakato mmoja kama kwa mwingine. Ni Bwana atendaye kazi katika fikra na kutengeneza tabia 



Wote hawaongozwi kwa Mwokozi kwa urahisi kwa njia moja. Wanadamu hawapaswi kufasili bila mantiki na kwa ufinyu, sifa za utendaji wa Mungu katika fikra. Anaweza kupewa mmoja kupata nguvu ya kiroho na utambuzi kwa urahisi, wakati ambapo mwingine analazimika kupambana na, “mwiba katika mwili” (2 Wakorintho 12:7), na kuna wakati yu tayari, kwa uwazi kabisa, kushuka kutoka katika vilele vya majabali. Hivyo ni nani anayethubutu kusema kwamba Mungu bado hampendi na kumchukulia kama mtoto wake yule anayeshambuliwa tu, na kwamba mkono wake bado haunyooshwi ili kuokoa? 



Mchungaji wa kimbingu anajua pa kuwapata wanakondoo waliotanga mbali na zizi. Atawakusanya awalete ndani. Huwaita wachungaji na washiriki walei kuamka na kutenda wajibu wao, na kuungana naye katika kazi hii. Ni jukumu la pekee la Mkristo kutafuta na kuokoa kilichopotea. Wachungaji na walei wanapaswa kuwatia moyo na kuwasaidia wale wanaosongwa na majaribu, pasipokujua ni njia ipi wageukie. Ndugu yangu, kupitia kwa neema ya Mungu unaweza kuwa anayewarudisha wanaotanga katika zizi. 



Kama katika siku za Eliya, Mungu alikuwa na watu elfu saba ambao hawakuwa wamemsujudia Baali, hivyo leo anao ulimwenguni wengi ambao wanatembea katika nuru waliyoipokea. Amejihifadhia kundi kubwa la waliochaguliwa, kwamba bado watadumu kuangaza katikati ya giza. Katika maeneo yanayoweza kutegemewa kuwa na waridi mwitu na miiba tu, mti uzaao matunda ya haki utaonekana. Katika maeneo kama haya wapo watakaochanua kwa utamu kwa ajili ya Bwana kuliko wengi wanaoishi katika maeneo mazuri. Kote kuwazunguka watasambaza harufu nzuri ya neema yake wakichanua katika maeneo yasiyotia matumaini ya ufanisi. 

No comments