mavazi katika UKRISTO
MAVAZI NI KITAMBULISHO CHA MTAKATIFU:
Kama sisi ni raia wa mbinguni na wakati wowote kuanzia sasa tunatarajia kunyakuliwa na Yesu mawinguni.
Wafilipi3:20
Hatuwezi kupuuza ukweli huu kwamba UTAKATIFU WETU, lazima uzingatie pia MAVAZI tunayovaa.
Kuna fundisho potofu linasema "MUNGU HAANGALII MAMBO YA NJE BALI ANATAZAMA NDANI YA MOYO".
Usipojua matumizi sahihi ya kila neno lililoandikwa kwenye Biblia utakuwa mwana wa Jehanamu unayeisubiri ghadhabu ya Mungu!
Maana anayekosesha inamfaa afungiwe jiwe zito shingoni na kutupwa kwenye kilindi cha bahari (Mathayo18:6)
Wahubiri vipofu wa vipofu Yesu anasema "SAFISHENI NDANI KWANZA ILI NJE NAYO IPATE KUWA SAFI"
Mathayo23:26.
Utakatifu ni NDANI na NJE
maana yake UTAKATIFU ni MWILI NA ROHO
soma (1Wakorinto7:34,2Wakorinto7:1)
Biblia imetupa mwongozo juu mavazi yatupasayo kuvaa wanaume kwa wanawake.
Mwanaume hapaswi kuvaa mavazi ya mwanamke wala mwanamke asivae mavazi ya mwanaume.
Maumbile yetu yanapaswa kutufundisha juu ya mavazi gani yatupasayo kuvaa.
Kumbukumbu22:5, 1Wakorinto11:14.
*Wako wahubiri wengine wanadai kwamba tuna uhuru wa kuvaa mavazi yoyote wakati huu wa NEEMA YA KRISTO!
Nataka niseme, wahubiri wa jinsi hiyo ni MANABII WA UONGO!
Kwani NEEMA YA KRISTO haitufundishi kufanya dhambi bali inatufundisha kukataa dhambi na tamaa za kidunia ili tupate kuishi kwa HAKI na UTAUWA katika ulimwengu huu wa sasa (Tito2:11-12).
MAVAZI YA KIKAHABA HAYAPASWI KUONEKANA KWA MTAKATIFU
Mithali7:10.
Mavazi ya kikahaba ni jumla ya mavazi yoyote yale yanayoweza kuchochea hisia za uasherati/uzinzi. Mavazi ya kikahaba zaidi sina huvaliwa na Wanawake ijapo kwa wanaume si sana.
Mavazi yoyote yanayoonesha utupu! Mavazi yoyote yanayobana (skin-tyte) na kuchora umbile la mtu! Magauni mafupi, Sketi zenye mpasuo! na mavazi mengine ambayo watu wanaokuona watadhania kuwa wewe ni kahaba hata kama umeolewa, hata kama wewe ni mwanakwaya, mama mchungaji nk.
angalia Biblia yako (Mwanzo38:15).
Kumbe mavazi unayovaa yanasehemu kubwa ya kukutambulisha kwenye jamii kuwa wewe ni nani au una tabia gani hata kama hauko hivyo!
Yesu anasema "Aibu ya uchi wako isionekane" Ufunuo3:18b.
Ndiyo maana mavazi haya ya uchi yanajulikana sana kama
MAVAZI YA AIBU, na wanapenda kuyavaa Makahaba wakiwa kwenye mawindo yao.
VAA MAVAZI YA KIBIBLIA KWA UTUKUFU WA MUNGU
ISAYA61:10, Kuna mavazi ambayo ukivaa yatakutambulisha kwenye jamii kuwa umeokoka.sasa mfn hii tabia ya Wanawake kuvaa Suruali za kubana Maungo yao Mungu amekataa,
Na hii itakusaidia wewe mwenyewe kutopata usumbufu wa kutongozwa-tongozwa ovyo mitaani, kazini, shuleni nk.
1Wakorinto10:31-33.
Kanisa la Mungu la kweli lazima mafundisho ya mavazi yafundishwe kwa nguvu sana hasa katika nyakati hizi za kizazi cha Kidigital! kizazi cha .com!
Lazima KANISA LA MUNGU litofautiane na dunia Warumi12:2, Wagalatia4:4, 1Yohana2:15-17. Ndo maana Ukisoma pia 1petro 3:3 pia nayo imefafanua Ni jinsi gani Wanawake wale wa zamani walikuwa wanapewa semina Ni namna gani ifaayo ktk muonekano wao wa nje Wasisuke NYWELE,na mengine yafananayo na hayo mfn kwa dunia ya Sasa dhambi ya kujipamba Shetani ameipanua zaidi Wanawake Kuvaa Shanga,Kukari NYWELE,Kukoboa ngozi ili Wawe weupe,Kuweka Tatoo,Kupaka Rangi za Midomoni,mpaka Wanaume Sasa nao Wamevamiwa nao Wanasuka, Ila Mungu alihimiza wajipambe utu ule wa ndani ili kumpendeza Mungu na wamewe 1temotheo 2:9, Isaya 3:16-24 Kwahiyo KUSUKA NYWELE nayo Ni dhambi inayouharibu ule utu wa ndani was kimungu ,baadhi ya Makanisa hutetea swala hili KUSUKA hivo wanapingana na MUNGU bila kujua Mungu awape kuona wageuke na kuacha maana Wachungaji ipo siku Mungu atawadai kuwapoteza Watu kwa upofu wa dhambi ya Kurahisisha Ni dhambi mbaya sana ifike hatua Wachungaji waseme ukweli na kuikemea dhambi waache kupenda kupokea sadaka tu huku Wakijua Kondoo wao Wanawakosesha kuwapeleka Jehanamu kwa kutowaambia Ukweli Ni Bora ukabaki.na Waumini Wachache Ila wenye kupokea Maonyo na Mafundisho na Kuyaishi NB mithali 28:13 2Timotheo 2:19 by Divinity Man
Post a Comment