amka na bwana leo 1

KESHA LA ASUBUHI

JUMATATU, MACHI, 1, 2021
SOMO: ULINZI PEKEE

Kisha, nena wewe na wana wa Israeli, na kuwaambia, Hakika mtazishika sabato zangu, kwa kuwa ni ishara ya mimi na ninyi katika vizazi vyenu vyote; ili mpate kujua ya kuwa mimi ndimi BWANA niwatakasaye ninyi. 

Kutoka 31:13



Hebu kila mmoja na amtafute Bwana kwa ajili yake mwenyewe. Milele iko mbele yetu. Usithubutu kuruhusu siku nyingine ipite bila kuchukua nafasi yako upande wa Bwana. Je, hutafanya sehemu yako ambayo Mungu amekuchagua kuifanya katika matukio ya mwisho ya historia ya dunia hii? 



Haiwezekani kutoa wazo lolote la uzoefu wa watu wa Mungu watakaokuwa hai duniani wakati ole zilizopita na utukufu wa mbinguni vitakapochangamana. Watatembea katika nuru itokayo katika kiti cha enzi cha Mungu. Kupitia kwa malaika kutakuwa na mawasiliano ya kudumu kati ya mbingu na dunia. Na Shetani, akizungukwa na malaika waovu, na akidai kuwa Mungu, atafanya miujiza ya kila namna, kudanganya, kama yamkini hata walio wateule. 



Watu wa Mungu hawatapata usalama wao katika kufanya miujiza; kwa kuwa Shetani anaweza kughushi muujiza wowote unaoweza kufanywa. Watu wa Mungu waliojaribiwa na kupimwa watapata nguvu yao katika ishara iliyotamkwa katika Kutoka 31:12—18. Wanapaswa kuchukua msimamo wao katika Neno lililo hai —"Imeandikwa" Huu ndio msingi pekee ambao wanaweza kusimama juu yake kwa usalama. Wale waliovunja agano lao na Mungu katika siku ile watakuwa bila tumaini na bila Mungu duniani. 



Wanaomwabudu Mungu watatofautishwa hasa kwa kuiheshimu amri ya nne —kwa kuwa hii ndio ishara ya uweza wake wa uumbaji, na ushaidi wa dai lake uchaji na heshima toka kwa mwanadamu. Waovu watatofautishwa kwa juhudi zao kukanyaga chini ukumbusho wa Muumbaji, kuadhimisha taasisi ya Rumi. Katika suala la pambano, Wakristo watagawanywa katika madaraja makuu mawili —wale wazishikao amri za Mungu na imani ya Yesu, na wale wamwabuduo mnyama na sanamu yake na kupokea chapa yake... 



Mitihani ya kutisha na majaribu vinawangoja watu wa Mungu. Roho ya vita inayachochea mataifa toka mwisho mmoja hata mwisho mwingine wa nchi. Lakini katika wakati wa taabu inayokuja —wakati wa taabu ambayo mfano wake haukuwapo tangu lilipoanza kuwapo taifa —watu wa Mungu waliochaguliwa watasimama bila kutetereka. Shetani na malaika zake hawawezi kuwaangamiza; kwa kuwa malaika wenye nguvu zaidi watawalinda. 

No comments