mafunzo ya watu wazima leo 1

LESONI, MACHI 1

SOMO: SHAIRI LA MTUMISHI ANAYETESEKA (ISAYA. 52:13—53:12)



Isaya 52:13—53:12, ijulikanayo kama “Shairi la Mtumishi Anayeteseka,” huthibitisha sifa ya Isaya kama "nabii wa injili." Katika kupatana na ubora wa injili, shairi huenda juu zaidi ya fasihi nyinginezo. Japo linashangaza kwa ufupi, kila kirai kimejawa maana muhimu inayofunua kiini cha safari ya Mungu isiyofikirika ya kutafuta kuokoa jamii ya wanadamu waliozama na kupotea dhambini. 



Haya sio “maziwa” ya neno la Isaya. Amewaandaa wasomaji wake kwa kujenga mada ya Masihi kuanzia sehemu ya awali ya kitabu chake. Kwa kufuata mwendo wa jumla wa maisha ya Masihi duniani, nabii alianza na kutungwa kwa mimba yake na kuzaliwa (Isa. 7:14), akaelezea utambulisho wake kama mfalme mtukufu atokaye katika ukoo wa Daudi (Isa. 9:6, 7), akafafanua kuhusu kazi yake ya urejeshaji kwa ajili ya Israeli (Isa. 11:1—16) na huduma ya kimya ya ukombozi kutokana na kukosa haki na mateso (Isa. 42:1—7). Kisha Isaya akafunua kwamba mfululizo wa matukio maalum ya Masihi hujumuisha msiba kabla ya kutukuzwa (Isa. 49:1—12, Isa. 50:6—10). Sasa Shairi la Mtumishi Anayeteseka hufikia katika kiini cha msiba. 



Rudi katika sehemu zile zilizoorodheshwa katika aya ya hapo juu. Pitia upya zinachotwambia kuhusu Masihi, Yesu. Zinasaidiaje kutuandaa kwa kile kinachokuja katika Isaya 52 na 53? Au zinafanya tu kile kinachotokea katika Isaya 52 na 53 kuwa cha kushtusha zaidi?



Isaya 52:13—53:1 hutoa utangulizi wa shairi na onesho la awali likiwa na tofauti nzuri mno: Mtumishi atasitawi na kutukuzwa, lakini mwonekano wake utaharibiwa hata asitambuliwe. Ni nani awezaye kuiamini? 



Isaya 53:2, 3 huanza kwa mshuko wenye maumivu kutoka kwa asili ya Mtumishi na mwonekano wa awali kufikia huzuni na kukataliwa kwake. Isaya 53:4—6 huweka kituo kuelezea kwamba mateso Yake kwa hakika ni yetu, anayobeba ili kutuponya. Isaya 53:7—9 huendeleza mshuko wa Mtumishi asiye na hatia hadi kaburini. 



Isaya 53:10—12, Mtumishi hupanda kufikia thawabu iliyotukuka iliyotabiriwa mwanzoni mwa shairi kuanzia katika Isaya 52:13, pamoja na uelewa zaidi kwamba kafara yake ili kuwaokoa wengine ni mapenzi ya Mungu. 



Linganisha shairi hili na muundo wa “bonde” wa Wafilipi 2:5—11, ambapo Yesu anaanza katika namna ya Mungu lakini anashuka akiacha utukufu na kutwaa namna ya utumwa wa mfano wa umbo la mwanadamu, akinyenyekea hata mauti: mauti ya msalaba. Kwa hiyo, tena Mungu humwadhimisha zaidi ili kwamba kila mmoja amtambue kama Bwana (linganisha Isa. 49:7). 



Soma Isaya 52:13—53:12. Andika kila kitu shairi linachosema kuwa Yesu ametutendea. Tafakari juu ya kile matendo hayo kwa niaba yetu yamaanishacho kwetu. 

No comments